Tuesday, 9 February 2010

Dk.Karume akutana na Mkuu wa Chuo Kikuu cha TunguuRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Amani Abeid Karume, akisalimiana na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tunguu,(Zanzibar University) Prof Muhamad Omar Zubeir, alipofika Ikulu Mjini Zanzibar .

Picha na Ramadhan Othman Ikulu.

Kamati Maalum ya Halmashauri kuu CCM yakutana


Makamo Mwenyekiti wa CCM, na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Amani Abeid Karume,(katikati) Mjumbe wa Kamati Kuu (NEC)na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Ali Mohammed Shein,(wapili kushoto)Mjumbe wa Kamati Kuu CCM na Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha,(kushoto),Rais Mstaafu wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi na Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar, Saleh Ramadhan Feruzi(wapili kulia) wakiimba wimbo wa Chama cha Mapinduzi kabla ya Makamo Mwenyekiti CCM Zanzibar kufungua kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, Afisi Kuu Kisiwandui Mjini Zanzibar.(Picha na Ramadhan Othman,Ikulu)

Dk.Karume akutana na Balozi wa Zambia


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume, akibadilishana mawazo na Balozi wa Zambia Nchini Tanzania, Darius Bubala aliyefika kujitambulisha jana, Ikulu Mjini Zanzibar.(Picha na Ramadhan Othman).