Wednesday 29 September 2010

DK. SHEIN: NITAJENGA MADARASA ZAIDI MSINGI.SEIKONDARI.

Jumatatu 27 Septemba



Dk. Shein: Nitajenga madarasa zaidi msingi, sekondari


l Wilaya ya kati kujengewa Kituo cha amali


l Barabara zilizobakia nazo kutengenezwa

lKukamilisha usambazaji maji, umeme Shehia zilizobakia

CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimeendelea kupokelewa na wananchi wengi zaidi, katika kampeni zake huku kikiahidi kuwapatia maendeleo makubwa yatayoweza kuleta mabadiliko ya maisha kwa wananchi wa wilaya ya kati Unguja jana, anaripoti MWANTANGA AME.

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk. Ali Mohammed Shein ameahidi hayo jana wakati akitoa sera za Chama cha mapinduzi kwa wananchi wa wilaya hiyo ikiwa ni muendelezo wa kampeni za Chama hicho kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, 2010.

Kampeni hizo jana zilifanyika katika Wilaya ya kati Unguja ambayo inayahusisha majimbo matatu likiwemo la Chwaka, Koani na Uzini, yakiwa na shehia 11.

Kampeni hizo zimeendelea kuonesha kuungwa mkono mgombea huyo baada ya makundi ya wanachama wa chama hicho na wananchi, kufurika katika kiwanja cha kampeni hizo Unguja Ukuu na kusababisha barabara ya Mkoa wa Kusini kuzidiwa kwa magari.

Akitoa sera za Chama hicho, Dk. Shein alisema wananchi na wanachama wa CCM wahakikishe wanakipa kura katika uchaguzi Mkuu ujao kwani ikiingia madarakani inakusudia kuendeleza barabara kadhaa za wilaya hiyo pamoja na kuinua sekta ya elimu, Kilimo, uvuvi na sekta ya Afya pamoja na huduma za jamii.

Akichambua mambo anayokusudia kuwamiminia wananchi wa wilaya hiyo, alisema ni pamoja na ujenzi wa barabara za Ukongoroni, Charawe, Ndijani, Jozani, Amani - Dunga, Koani-Jumbi, Kizimbani-Kiboje, Jendele-Cheju, na Njia nne Umbuji hadi Uroa, zitajengwa kwa kiwango cha lami.

Kuhusu sekta ya Afya, alisema Chama cha Mapinduzi kwa wilaya hiyo, inakusudia kuwaongezea ujenzi wa vituo vya afya kwa baadhi ya maeneo ambayo bado hayajawa na vituo hivyo yakiwemo ya kijiji cha Kikungwi kwa kuanzia.

Alisema katika sekta hiyo pia serikali ijayo ya awamu ya saba, itakuwa na mengi ya kuwatekelezea wananchi wa jimbo hilo katika kuandaa mpango mpya wa kuwa na Hospitali ya Wilaya na Mkoa kwa kuipatia vifaa muhimu.

Aidha kazi hiyo itaenda sambamba pamoja na kuweka vifaa vya uchunguzi katika hospitali hizo na kupambana na maradhi mazito yakiwemo ya ugonjwa wa Ukimwi, Malaria na Kifua Kikuu.

Upande wa sekta ya elimu, Dk. Shein aliahidi kuwa akiwa madarakani atahakikisha kunakuwa na mabadiliko katika sekta hiyo kwa kuongeza madarasa ya kusomea ili kupunguza idadi ya wanafunzi katika darasa moja kwa kufikia 40 badala ya hivi sasa kuwa katika idadi ya wanafunzi 60.

Akiendelea alisema katika Skuli hizo ambazo zitajengwa sambamba na nyumba tatu za walimu pia serikali hiyo itajenga skuli mbili za sekondari za wilaya ambazo zitajengwa katika kijiji cha Uzini na Koani, zitakuwa na vifaa vya maabara zitazokuwa za kisasa pamoja na vitabu vya kusomea kwa kila mwanafunzi.

Eneo jengine ambalo amelitaja ni la ujenzi wa Skuli za Amali pamoja na vituocha Elimu Mbadala ambavyo wananchi wa wilaya hiyo wataweza kuvitumia kwa kuongeza viwango vya elimu.





Ccccccccc

No comments:

Post a Comment