Wednesday 29 September 2010

MAALIM SEIF AUSUSA MKUTANO KAMPENI

Maalim Seif aususa mkutano kampeni



Ni kwa kujitokeza wanachama ‘kiduchu’

KWA mara ya kwanza tokea kuanza kwa historia ya vyama vingi vya Siasa Tanzania , Katibu Mkuu wa CUF, Malim Seif Sharif Hamad, amekataa kuwahutubia wafuasi wa Chama hicho akatika Jimbo la Chake Chake Kisiwani Pemba kwa kutoridhishwa na mahudhurio.

Maalim, alikuwa mgeni Rasmi katika Mkutano huo uliofanyika katika Kiwanja cha Banda Taka , Jimbo la Chake Chake , kwaajili ya kuwanadi Wagombea Ubunge na Uwakilishi wa Jimbo hilo.

Katibu Mkuu huyo alisema ni vyema mkutano huo, ukapangwa siku nyengine tena iwe jioni na asubuhi kama ilivyokuwa ambapo alisimama jukwaani kwa muda wa dakika 10.

“Siridhiki na na wtu waliojitokeza na idadi ya watu wa Jimbo la Chake Chake , na muomba meneja wa Kampeni anipangie mkutano mwengine tena iwe jioni”, alieleza Maalim Seif.

Hata hivyo aliwanadi wagombea wa Ubunge , Uwakilishi , na Udiwani wa Wadi za Chake Chake na kuwataka wananchi kuwapa kura zao iliwaijenge Chake Chake mpya na baadae kuteremka katika jukwaa hilo.

Pamoja na kiroja hicho cha mwanzo kutokea katika mikutano ya Maalim Seif hapa Pemba , lakini baadhi ya wananchi walisikika wakisema kuwa uzembe ulifanyika katika kuutangaaza mkutano huo kwa viongozi husika wa CUF, ambao ulipaswa kutangazwa Pemba nzima ijapo kuwa ni wajimbo.

Hivyo pamoja na mgombea huyo kukataa kuhutubia Wafuasi wake , lakini Mjumbe wa Baraza kuu la Cuf, Taifa na mwakilishi wa Chama hicho alikuwa akimnadi Mgombea huyo wa Urais kwa tiketi ya CUF, kwa kuwataka Wananchi wa Pemba kumpa kura zao maalim Seif

No comments:

Post a Comment