Wednesday 29 September 2010

UGENI MKONO MARIDHIANO YA CCM, CUF :HAMADI

Ungeni mkono maridhiano ya CCM, CUF: Hamad

MGOMBEA uraisi wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Maalim Seif Sharif Hamadi amewataka Wazanzibari kuunga mkono maridhiano baina yake, Katibu Mkuu wa CUF na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Amani Abeid Karume ili kuishi kwa umoja na maelewano, anaripoti SHAIB KIFAYA.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni wa CUF uliofanyika viwanja vya Kombawapya, Mgombea huyo alisema hatakuwa tayari kuona maridhiano hayo yanachezewa hali ambayo kamwe haitaashiria amani na utulivu.

Alisema jambo muhimu lililobaki hasa katika kuelekea katika uchaguzi mkuu ujao ni kuijenga Zanzibar mpya iliyojaa neema kwa maslahi ya taifa na wananchi wa jumla.

Akizungumzia kuhusu maendeleo ya Zanzibar, Maalim Seif alisema endapo atapewa fursa ya kukikalia kiti cha Urais wa Zanzibar atahakikisha kuwa wananchi wake wanaondokana na kero nyingi zinazowakabili chini ya utawala wa kisheria.

Kuhusu suala la ajira, alifahamisha kuwa Zanzibar mpya itafungua milango ya uwekezaji wa viwanda ili vijana waweze kujiajiri na kufungua masoko katika nchi za nchi kwa lengo la kukabiliana na umasikini nchini.

Aidha ameahidi kuwa serikali atakayoiongoza itakuwa na ushirikiano wa karibu sana na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kuwahakikishia wananchi wa pande zote mbili maisha ya salama kwa kuondosha kero za Muungano huo.

Alisema ni vyema wananchi wakaishi kwa amani na maridhiano kupitia viongozi wao ambao ndio wanaowategemea kutatua matatizo

No comments:

Post a Comment