Monday 4 October 2010

148/= ZATUMIKA IJENZI BUSTANI YA JAMUHURI WELESI.

148m/- zatumika ujenzi bustani ya Jamhuri


Na Halima Abdalla
4 OCTOBER 2010

KIASI cha shilingi milioni 148 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa uzio na uboreshaji wa bustani katika eneo la bustani ya Jamhuri.

Aidha shilingi milioni 48 zimetumika kwa ajili ya kununua mapembea kwa ajili ya kuchezea watoto katika kiwanja hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja Muendeshaji wa kiwanja hicho, Ali Abdalla Ali, alisema lengo la kutengeneza bustani hiyo ni kuwawezesha watoto kupata fursa ya kufurahia hazi zao za msingi kwa kushirikiriana na wenzao kwa kucheza na kuendeleza michezo ya watoto sambamba na kuimarisha bustani hiyo.

Alieleza kuwa endapo watapatiwa eneo jengine linaloweza kutumiwa kwa malengo kama hayo wako tayari kuliimarisha kwa ajili hiyo.

''Tumeamua kuwekeza katika nchi yetu si lazima kila siku wawekeze watu kutoka nje hata sisi wenyewe tunaweza kuwekeza", alisema.

Nae Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa,Rashid Juma alisema tokea kuboreshwa kwa bustani hiyo kiasi cha vijana 30 wazalendo wameajiriwa kwa shughuli za bustani katika eneo hilo.

Rashid alisema duniani kote watu wameweza kujiletea maendeleo kwa kubadilisha mandhari katika sehemu za kupumzika na wamefanikiwa kiuchumi ikiwemo kupata ajira.

Sambamba na hayo alisema Baraza la Manispaa lina mpango wa kuboresha pia bustani ya Donge, Gofu na maeneo mengine ili kuendana na wakati.

Alisema kuna maendeleo mengi yaliyofikiwa vijana ikiwa ni pamoja na kupungua wimbi la watoto kupotea tokea kujengwa kwa bustani hiyo ambapo watoto wengi wamekuwa wakifurahia kufika hapo na kucheza na wazazo wao kuwafuata baadaye kwa kuwarejesha nyumbani.

Aidha alisema kuwa maeneo ya maegesho ni sehemu nyengin muhimu ambayo inazidi kuupa mji sura ya kuvutia.

''Haya ni mambo mazuri kwa nchi yetu mafanikio mengi tunayo lakini watu hawaoni utakuta mtu anakaa pembeni na kuzungumza bustani imeharibiwa hawaoni haya mafanikio? ", alihoji.

Sambamba na hayo aliwataka wananchi kuyatunza maeneo hayo ili yaweze kudumu na kama kunawatu wengine wa ndani ya nchi wanataka kuwekeza nafasi zipo watapatiwa maeneo mengine.

No comments:

Post a Comment