Kidato cha nne waanza mitihani leo
Na Mwandishi wetu
4 OCTOBER 2010
MITIHANI ya kidato cha nne inafanyika nchini kote leo huku Baraza la Mitihani la Taifa, NECTA, likiwaondoa watahiniwa 1,376 wa kujitegemea na 1,487 wa skuli.
Wanafunzi hawatafanya mitihani kutokana na kubainika kuwa na kasoro kadhaa zikiwemo kutokuwa na matokeo sahihi ya mtihani wa kidato cha pili.
Taarifa ya NECTA pia imesema watahiniwa 2,124 walioomba kusajiliwa kama watahiniwa wa skuli wamesajiliwa kama watahiniwa wa kujitegemea baaa ya kubainika kuwa hawana sifa za kuwa watahiniwa wa skuli.
Uongozi wa Shirika la Magazeti ya Serikali na wafanyakazi wanawatakiwa wanafunzi wote mitihani mema.
Monday, 4 October 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment