Sunday 3 October 2010

DANGURO JENGINE LAVUMBULIWA MALINDI.

Danguro jengine lavumbuliwa Malindi

Na Waandishi Wetu
1 october 2010.
WIKI chache baada ya uchunguzi wa Zanzibar Leo kubaini kuuzwa chakula mchana wa Ramadhani eneo liliyopo pembezoni ya soko la samaki Malindi mjini hapa, kadhia nyengine mpya ya ufuska imeibuka katika eneo hilo.

Uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa eneo hilo ambapo kuna banda linalomilikiwa na shirika moja limegeuzwa kuwa danguro.

Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali vya habari vilivyohojiwa na gazeti hili vimeeleza kuwa danguro hilo linaendeshwa na mtu mmoja anayejulikana kwa jina maarufu Jiti.

Bwana huyo amekuwa akiendesha shughuli za matendo machafu katika eneo hilo ambapo amekuwa akichukua makahaba maarufu wa kiume kutoka sehemu mbali mbali hapa nchini.

Baadhi ya wafanyabiashara wa samaki walilieleza gazeti hili kuwa wamechoshwa na vitendo hivyo vilivyo kinyume na maadili vinavyofanywa na mtu huyo ambaye amekuwa tishio.

"Tumefurahi sana leo mmekuja kuzitafuta habari hizi, hili eneo lina habari nzito unaliona hilo banda hapo, hilo si banda bali ni danguro la makahaba wa kiume wanaoingizwa na kufanya vitendo vichafu",alieleza mmoja kati ya wafanyabiashara katika eneo hilo.

Alifahamisha kuwa baadhi ya watu wanaokuja kufanywa mambo hayo kwenye danguro hilo, hutolewa nje ya Zanzibar.

Mmoja wa maofisa wa shirika hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe alithibitisha kuwepo kwa vitendo hivyo kwa muda mrefu sasa.

"Mbona haya mambo yapo zamani watu wote wanajua, cha kushangaza hata baadhi ya askari polisi katika vituo vya karibu wanajua kinachoendelea kwenye banda hilo", alisema Afisa huyo.

Afisa huyo alishindwa kutoa maelezo zaidi juu ya kadhia ya matendo machafu yanayoendelea kwenye eneo hilo, akisema kuwa yeye si msemaji na haelewi kama Shirika lake limempa eneo hilo Jiti.

Aidha katika eneo jengine lililopo karibu na eneo hilo ambalo linajulikana kwa jina maarufu la Kwamapaka ambako nako kuna mabanda nako kunaendeshwa biashara ya ngono kwa madada poa.

Mbali ya shughuli hizo za ngono pia eneo hilo limekuwa likifanyika biashara haramu ya dawa za kulevya.

Sheha wa Shehia ya Malindi, Himid Omari alilithibitishia gazeti hili kuwa anazo habari za kuendelea kwa matendo hayo machafu kwenye shehia yake.

No comments:

Post a Comment