Monday, 4 October 2010

VIFAA VYA KURA KUWASILI MWISHONI MWA MWEZI.

Vifaa vya kura kuwasili mwishoni mwa mwezi


Na Mwantanga Ame
2 0CTOBER 2010

TUME ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), imesema vifaa vya kupigia kura kwa uchaguzi mkuu utaofanyika mwishoni mwa mwezi huu vitawasili nchini Oktoba 26.

Afisa Uhusiano wa ZEC, Idrisaa Haji Jecha alisema hayo alipokuwa akizungumza na Zanzibar Leo huko Afisini kwake Maisara mjini Zanzibar.

Alisema vifaa vyote vitakavyotumika kwenye uchaguzi mkuu zikiwemo karatasi zitawasili nchini sikui huyo vikitokea nchini Afrika Kusini ambako ndoko viliko tengenezwa.

Aidha lifahamisha kuwa kwenye vifaa hivyo pia Tume inakamilisha kupata vifaa muhimu vitavyowawezesha kupiga kura kwa watu wasioona kumudu kupiga kura wenyewe bila ya kupata msaada wa mtu mwengine.

Alisema Tume imelazimika kuchukua hatua hiyo baada ya baadhi ya wapiga kura katika Jumuiya ya Wasioona kulalamikia kuandaliwa mazingira yatayowawezesha kupiga kura bila msaada wa mtu mwengine.

Alisema ingawa Jumuiya hiyo haikuwasilisha malalamiko yao hayo rasmi kwa tume ya uchaguzi, lakini Tume imeyapokea kupitia vyombo vya habari jambo ambalo imelizingatia na kulifanyikazi.

Alisema hapo awali Tume ilishindwa kutoa tamko juu ya suala hilo kwa vile walikuwa wakisubiri kukamilika kwa mchakato wa zoezi la uchukuaji fomu ili kupata wagombea halisi kwa ajili ya kuandaa karatasi za kupigia kura.

Alisema kupatikana kwa vifaa vitakavyowawezesha watu wasioona kupiga kura itakuwa jambo la msingi ambapo walemavu hao wataweza kuwatambua wagombea hao.

Afisa huyo alisema kazi kubwa ambayo wanatarajia kuifanya baada ya kuwapatikana kwa kifaa hicho ni jinsi ya kuwapa elimu walemavu hao ili waweze kutambua namna ya kukitumia wakati uchaguzi utakapowadia.

No comments:

Post a Comment