Monday 4 October 2010

PBZ YAAHIDI KUSAMBAZA ATM KILA KONA.

PBZ yaahidi kusambaza ATM kila kona



Na Zulekha Saleh
3 OCTOBER 2010, JUMAPILI

BENKI ya watu wa Zanzibar PBZ imesema kuwa ina mipango ya kueneza huduma ya ATM, katika maeneo yote ya Tanzania ili wateja wake waweze kuchukua fedha popote waliopo.

Katika kusambaza huduma hiyo PBZ, inatarajia kufungua vituo vyengine zaidi katika maeneo ya Mlandege kwa Unguja,Chake chake,Wete na Mkoani kwa Pemba.

Akitoa maelezo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Juma Amour alisema wanatarajia kufungua vituo vyengine Tanzania bara ili huduma ya hiyo iweze kuenea Tanzania nzima.

''Tuna mpango wa kufungua vituo Tanzania nzima hadi Tanzania bara ili wateja wetu wote wafaidike na huduma hii'', alisema.

Aidha PBZ ina mpango wa kutoa vipeperushi ambavyo viko katika matayarisho vitakuwa vikitoa maelekezo yanayoelekeza jinsi ya kutumia huduma hiyo.

''Katika kuelekeza namna ya kutumia huduma hii tunatayarisha vipeperushi ambavyo vitakuwa vikielekeza namna ya kutumia huduma hiyo,''alifafanua.

Kadi ya SPICE inayotolewa na Benki ya watu wa Zanzibar ambayo inamuwezesha mteja wa Benki hiyo kupata huduma za ATMs zilizounganishwa na mtandao wa 'Umoja Swich'popote pale Tanzania.

Mteja yeyote wa Benki ya watu wa Zanzibar mwenye akaunti ya akiba au ya biashara anaweza kupata kadi ya SPICE kwa kiwango kidogo cha pesa.

No comments:

Post a Comment