Monday 4 October 2010

USTAWI WA JAMII KUYAPATIA UFUMBUZI MATATIZO YA WAZEE.

Ustawi wa Jamii kuyapatia ufumbuzi matatizo ya wazee

Na Fatma Kassim, Maelezo

2 OCTOBER 2010 
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar, imesema kuwa inazitambua vyema shida na matatizo yanayowakabili wazee, huku ikiyafanyiakazi bila ya kuwabagua.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ustawi wa Jamii, Ahmed Awadh alieleza hayo alipokuwa akizungumza na wazee katika maadhimisho ya siku ya wazee duniani yanayoadhinishwa kila ifikapo Oktoba Mosi.

Alisema matatizo yanayowakabili wazee ni mengi ambayo yamegawika katika makundi tofauti, yakiwemo yanayowakumba wafugaji, wakulima, na wastaafu mara baada ya utumishi kumalizika na serikali bado inathamini mchango wao walioutoa katika taifa.

Alifahamisha kuwa juhudi zaidi zinafanywa ili kuhakikisha kundi hilo katika jamii yanasaidiwa ili yaweze kuondokana na matatizo yao.

Aidha alisema kutokana na umuhimu wa wazee serikali inatoa kipaumbele masuala mazima ya kuwapatia hifadhi ikiwamo makaazi bora sambamba na huduma muhimu.

Nao wazee hao wamesema kutokana na kupanda maisha na mahitaji yanaongezeka wameomba kuongezewa posho lao la mwezi kufikia 50,000 pamoja na kupatiwa huduma muhimu.

Mapema Mwenyekiti wa kamati ya ufundi wa jumuiya ya wastaafu Zanzibar (JUWAZA), Aboud Talib alisema wazee wana mengi wanayoyahitaji yakiwemo huduma za afya, makaazi bora pamoja na kupewa posho ambalo litatua matatizo yao.

No comments:

Post a Comment