Sunday, 27 February 2011

Mashabiki Gor Mahia wavunja pambano

  Mashabiki Gor Mahia wavunja pambano

NAIROBI, Kenya

VURUGU za mashabiki katika viwanja vya soka zimeendelea kushuhudiwa, kufuatia wapenzi wa klabu ya Gor Mahia kuvamia uwanja wa Nyayo wakishindwa kuvumilia kipigo mikononi mwa Rangers katika ligi kuu ya nchi hiyo mwishoni mwa wiki.

Kutokana na ghasia hizo, muamuzi wa pambano hilo alilazimika kulivunja katika dakika ya 79 ambapo Gor Mahia ilikuwa nyuma kwa magoli 3-0.

Hapo kabla, mashabiki hao walianza kurusha vitu uwanjani zikiwemo chupa na mawe katika robo saa ya mwisho baada ya kuona timu yao ikipokea kipigo kizito, kabla kuvunja uzio na kujitosa uwanjani huku baadhi yao wakiushambulia ubao wa matokeo.

Askari wa Jeshi la Polisi walilazimika kufyatua mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya mashabiki hao.

Muamuzi wa mchezo huo Davis Omweno, hakuwa na njia nyengine bali kuuvunja mpambano huo ambao kabla kitendo cha wapenzi wa Gor Mahia ulikuwa mzuri huku timu zote zikicheza kiungwana.

Mtendaji Mkuu wa Ligi Kuu ya Kenya, amekilaani kitendo hicho na kuahidi kuchukua hatua kali kwa waliohusika. (Nation).No comments:

Post a Comment