Thursday 19 August 2010

OMAN, ZANZIBAR ZASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO UTAMADUNI

Oman, Zanzibar zasaini mkataba ushirikiano utamaduni


Na Mwandishi wetu

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Oman zimetiliana saini mkataba wa makubaliano katika mambo ya Utamaduni, Makumbusho, Nyaraka na Mambo ya Kale.

Hafla ya utilianaji saini makubaliano hayo, ulifanyika katika ofisi za Wizara ya Elimu, Mazizini, Zanzibar kati ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali na Balozi mdogo wa Oman nchini Tanzania.

Akizungumza mara baada ya makubaliano hayo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Haroun Ali Suleiman alisema serikali inathamini michango inayotolewa na serikali ya Oman katika nyanja mbali mball katika kuisaidia Zanzibar.

Alisema utamaduni na historia ni muhimu sana katika nchi kwani ndio zenye kusaidia kuweka haiba nzuri ya nchi pamoja na kuleta umoja na mshikamano, udugu wa maendeleo na mambo mengine yanayoweka kumbukumbu za nchi.

Aidha alisema kuwa maelewano na ushirikiano baina ya Oman na Zanzibar ni ya siku nyingi hivyo, upo umuhinu wa kuyadumisha kwani historia na utamaduni wake vinalingana sana kutokana na kuwepo kwa historia ambayo inaelezea kuwepo mambo mbali mbali ya zamani kwa kla upande.

Alieleza kuwa serikali itashirikiana katika mambo ya elimu pamoja na mambo ya kale ili iweze kuyaendeleza na kudumisha historia nakuhakikisha kuwa makataba huo unatekelezwa kama ulivyokusudiwa.

Nae Balozi mdogo wa Oman, Majid Abdalla Al Abbadi ameishukuru serkali Zanzibar kwa ushirikiano wake na wataendelea kusaidia na kuendeleza makubaliano hayo.

Aidha alisema makumbusho ya Zanzibar ni muhimu sana na kivutio kikubwa katika nchi na ipo haja ya kuyadumishwa na kuweka historia nzuri na kumbukumbu sambamba na kuyafanyia matengenezo majengo yazamani yaweze kuwa kivutio zaidi.

Aidha alisema kuwa makubaliano hayo yatasaidia kubadilishana fikira, kielimu, matembezi pamoja na makundi ya Kiutamaduni ili kudumisha makubaliano hayo.

No comments:

Post a Comment