'WAANDISHI BADO MNAMAJUKUMU MAKUBWA KUFANIKISHA UCHAGUZI'
Na Halima Abdalla
MKURUGENZI wa Televisheni Zanzibar ,Chande Omar amesema bado waandishi wa bahari wanamajukumu makubwa katika kufanikisha chaguzi nchini kwa vile kazi yao ni muhimu katika wakati wote na zaidi kipindi cha Uchaguzi Mkuu.
Chande aliyasema hayo jana alipokuwa akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusiana na kuripoti habari za uchaguzi yaliowashirikisha waandishi wahabari kutoka vyombo mbali mbali vya Zanzibar.
Alisema kuwa mafunzo hayo yamekuja muda muafaka kwa waandishi kwani yataweza kuwasaidia katika kukusanya habari katika kipindi cha uchaguzi.
Alisema waandishi wa habari wanakabiliwa na changamoto kubwa katika kipindi hiki cha Uchaguzi, hivyo kupatiwa mafunzo hayo kutasaidia kwa kiais kikubwa katika kazi zao.
Sambamba na hayo, amekipongeza Kituo cha Dochi Velle kwa kuandaa mafunzo hayo yenye lengo la kuwasaidia waandishi wa habari wa Zanzibar.
Alisema wandishi wa habari ni watu muhimu na kwamba lazima kazi yao waifanye kwa kuzingatia maadili, mipaka na wawe wenyeuwezo katika kuitumia vizuri kalamau yao.
Nae Meneja wa Mpango wa mafunzo hayo, Kanda ya Afrika, Charles Achaye Ddong ,alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwaandaa waandishi wa habari Zanzibar kuweza kuripoti habari za Uchaguzi katika Kipindi cha Uchaguzi.
Aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kuwa makini wakati wa mafunzo hayo kwani yatawasaidia kwa kuwapa uwezo mkubwa zaidi wa kuandika habari kwa usahihi na umakini zaidi.
Mafunzo hayo ya siku tano yameandaliwa na Kituo cha DochiVelle cha Ujerumani ikishirikiana na Television Zanzibar.
No comments:
Post a Comment