Sauti ya Umma sasa chapata mgombea Urais Z'bar
Na Kassim Kassim, (TUDARCO)
HATIMAE Chama Cha Sauti ya Umma kimefanikiwa kusimamisha mgombea kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar katika Uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31.
Mgombea aliesimamishwa na Chama hicho, Haji Mussa Kitole ambae alikabidhiwa fomu za kuwania nafasi hiyo, jana 3:33 asubuhi na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Khatib Mwinyichande.
Haua ya kukabidhiwa fomu mwanachama huyo wa Sauti ya umma ilifikiwa baada ya kushindikana juzi kulikotokana na kujitokzea wanachama wawili badala ya mmoja kama taratibu zinavyotaka.
Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Salum Kassim Ali aliwarudisha na kuwashauri kutafuta muafaka ili mmoja wao aendelee na mchakato wa kuchukua fomu.
Chama hicho juzi kilishindwa kupewa fomu baada ya wagombea wawili wa chama hicho kujitokeza kudai fomu hizo.Waliojitokeza ni Haji Ramadhan Haji na Haji Mussa Kitole.
Aidha Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, akifafanua kuhusu sababu ya kumpatia fomu mgombea huyo, alisema inatokana na Chama Cha Sauti ya Umma kuiandikia barua Tume siku iliofuata iliosainiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho ikieleza kwamba Kitole ni chaguo la Chama hicho kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar.
Nae Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Khatib Mwinyichande alimpa pole Kitole kutokana na mzozo uliotokea juzi afisi ya Tume na kusababisha kusita kwa zoezi la utoaji fomu za kuwania Urais kupitia chama hicho.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi alimuomba mgombea huyo kufuata maelekezo ya na muongozo wa ujazaji fomu hiyo.
Zoezi la uteuzi wa wagombea Urais Zanzibar linatarajiwa kufanyika Septemba 2, 2010 katika afisi za Tume hiyo.
Wednesday, 18 August 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment