Shamuhuna atilia mkazo wanandoa kupima kabla kuoana
Na Hamad Hija, Maelezo
NAIBU Waziri Kiongozi na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Ali Juma Shamuhuna amewataka wananchi waliopata mgao wa vitabu vilivyotolewa na Taasisi ya Kiswahili na Lugha za kigeni kupitia CHAKUWAZA wavisome ili wapate maarifa yaliomo.
Shamuhuna aliyasema hayo jana huko Taasisi ya Kiswahili na lugha za Kigeni Zanzibar, wakati akizindua vitabu sita vya fasihi, vikiwemo vitabu vya tubadilike na kinga uzi ni vitabu vinavyozungumzia masuala ya kupambana na virusi vya ukimwi pamoja na ukimwi.
Alisema wananchi wanapaswa kuvisoma ili wafaidike na taaluma kubwa iliomo ndani yake, ikiwemo suala ya ukimwi na kwamba vitawapa wasomaji muongozo wa kupamba na ukimwi.
“Nakushaurini mvisome vitabu kwa vile kitu kilichoandikwa kama kitabu ni kwamba mawazo yake yanakuwa yanaganda katika mawazo ya watu na hivyo, kusaidia kufikisha ujumbe wa kile ambacho mtu amekisoma kwa kuwa hakitatoa haraka,” Alifafanua Shamuhuna.
Katika hafla hiyo ya uzinduzi wa vitabu hivyo sita vya fasihi ambavyo vimetungwa na Wazanzibari, Waziri Shamuhuna, alihimiza vijana kupima kwanza na ndipo wafunge ndoa kwa vile wanakuwa na uhakika wa usalama wa maisha yao.
Alisema ugonjwa wa ukimwi unaathiri nguvu kazi za taifa hivyo, ni vyema watu wakapima kabla ya kuoana ili kujua hali za afya zao mapema na sio kusubiri hadi nguvu kazi za jamii zikaathirika
Pia Shamuhuna, aliwataka watunga vitabu kuendelea na kazi yao kwa kuwa ni ya ujasiri kwa kutungu vitabu la kujenga mjajina yao na kuweza kuongeza uywezo wao katika kutunga.
Naye Mkurugenzi wa Tume ya Ukimwi ya Zanzibar (ZAC), Asha Abdulla, alisema Taasisi za kidini zina umuhimu mkubwa katika kupamba na ukimwi hivyo, zinawajibika kuendelea kutoa elimu hiyo kwa nmjia mbali mbali katia jitihada za kupambana na maradhi hayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment