Wednesday 1 December 2010

GADAFI ATAKA USHIRIKIANO AFRIKA, ULAYA.

Gadafi ataka ushirikiano Afrika, Ulaya



Na Rajab Mkasaba, Libya

RAIS wa Libya Muamar Gadafi amesema kuwa Afrika na Ulaya zina historia ndefu katika kukabiliana na changamoto za kimaendeleo.

Kiongozi huyo wa Libya alisema hayo kwenye ufunguzi wa mkutano wa tatu baina ya viongozi wakuu wa nchi za Afrika, Jumuiya ya Ulaya unaondelea nchini Libya.

Gadafi kutoka na historia hiyo wakati umefika kwa nchi za Ulaya kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati yake ya Afrika katika kuimarisha sekta za maendeleo na kukabiliana na tatizo la umasikini.

Alisema ushirikiano baina ya Ulaya na Afrika ni jambo muhimu hasa katika nyanja za kiuchumi na kama dhamira ya dhati itakuwepo watu wa sehemu hizo ndio watakaofaidia na ushirikiano huo.

Alisema licha ya kuwepo kwa changamoto mbali mbali zinazoikabili bara la Afrika, Ulaya ikiwemo ile ya kupambana na ugaidi, bado ushirikiano baina ya pande hizo unahitajika sambamba na kuzikabili changamoto hizo kwa pamoja.

Gadafi alisema Afrika ni bara lililojaaliwa kwa na rasilimali nyingi za kiuchumi lakini ili ziweze kuwa na tija ni lazima pawepo mikakati ya kuhakikisha bara hilo linapiga hatua katika kuviimariha vyanzo hivyo.

Rais huyo wa Libya aliwaeleza viongozi wa Ulaya kuwa suala la wakimbizi wengi wanaomiminika barani Ulaya kupitia katika nchi hiyo linaweza kudhibitiwa endapo atapewa ushirikiano mzuri.

Katika mkutano huo ambapo Tanzania inawakilishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein ulioanza juzi nchini Libya.

Mkutano huo wa siku mbili unaofanyika mjini Tripoli, Libya, umehudhuriwa na zaidi ya viongozi wakuu 80 wa nchi mbali mbali, ambapo mambo kadhaa yamejadiliwa yakiwemo suala zima la siasa, usalama, mabadiliko ya hali ya hewa, maendeleo ya sekta binafsi, miundombinu, umeme, kilimo, sayansi, ICT, usalama wa chakula na uhamiaji.

No comments:

Post a Comment