Friday 3 December 2010

RAIS KIKWETE ATEUA MAKATIBU TWALA WA MIKOA.

Rais Kikwete ateua makatibu Tawala wa Mikoa







Kawthar Iss-hack, Dar es Salaam


Ijumaa 3 Disemba 3010


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amewateua Makatibu Tawala wa Mikoa ya Arusha, Kagera, Morogoro, Singida,Tanga na Tabora ili kujaza nafasi za waliostaafu na wale walioteuliwa kushika nafasi za juu serikalini.

Walioteuliwa ni Evelyne Itanisa anayekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha ambaye anachukua nafasi ya Nuru Millao amabye kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii

Mwingine ni Nassor Mnambila ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera ambaye anachukuwa nafasi ya Bilia ambaye aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.

Aidha katika uteuzi huo pia Rais Jakaya Kikwete amemteuwa Mgeni Suffiani Baruani kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro anayechukuwa nafasi ya Hussein Katanga ambaye aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto.

Nae Liana Ayubu Hassan ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida ambaye amechukuwa nafasi ya Godfrey Ngaleya ambaye amestaafu utumishi wa umma.

Aidha Rais Kikwete amemteuwa Benedict Ole Kuyan, kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga ambaye amechukuwa nafasi ya Paul Kichira ambaye amestaafu katika utumishi wa umma.

Naye Mwinyimvua ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora ambaye amechukuwa nafasi ya Theresia Mmando ambaye amehamishiwa Mkoa wa Dar es Salaam kushika nafasi ya Assumpta Ndimbo ambaye anastaafu katika Utumishi wa Umma.

Wakati huo huo, taarifa kutoka Ikulu mjini Dar es Salaam imeeleza kuwa Chama cha Wanasheria wanawake Tanzania (TAWLA) kimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuchaguliwa kuiongoza Tanzania.

TAWLA kimesema ushindi alioupata Rais Kikwete katika Uchaguzi Mkuu uliopita ni zawadi na dhamira ya dhati ya kuwatumikia Watanzania. “Kwa kukuchagua wewe, Watanzania wamechagua maendeleo, uwazi na uhakika,” kimesema chama cha TAWLA katika taarifa yake.

Chama hicho kimemuhakikishia Rais Jakaya Kikwete kuwa kitaendelea kutoa ushirikiano kwake na kwa Serikali yake ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika jitihada za kuleta maendeleo ya nchi yetu.

No comments:

Post a Comment