Tuesday 13 April 2010

Dk.Karume afanya uteuzi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.. Amani Abeid Karume amemteua Khamis Mussa Omar , kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee jana, uteuzi wa Khamis Mussa unaanzia April 9, 2010 .

Khamis Mussa hivi sasa ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi Zanzibar.

Aidha, Rais Karume amemteua Ali Mzee Ali kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri katika Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu, Zanzibar.

Uteuzi wake unaanzia April 9, 2010.

Ali Mzee Ali ni Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa kuteualiwa na Rais .

Aidha anashikilia nafasi ya Mweyekiti wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

No comments:

Post a Comment