Saturday 10 April 2010

Matumizi mabaya rasilimali yachangia mabadiliko hali ya hewa

Na Zuwena Shaaban, Pemba
IMEELEZWA kuwa matumizi mabaya ya rasilimali yanayosababisha kuongezeka kwa kasi mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

Matumizi hayo ni pamoja na ukataji miti, utumiaji mbaya wa fukwe za bahari, utumiaji wa vyazo vya maji visivyo stahiki hupelekea kuongozeka kwa joto duniani na kupanda juu kina cha maji ya bahari na kutoboa tabaka la juu la ozoni.

Hayo aliyasema Kaimu Afisa Mdhamini Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Pemba, Ismail Ali Juma, alipofungua semina juu ya athari ya maji taka iliyofanyika ukumbi wa Kiwanda cha mafuta ya Makonyo Wawi Chake Chake Pemba.

Aliezea kuwa utumiaji wa maji taka huathiri mambo mbali mbali kwa mwanadamu na viumbe vyengine.

Alifafanua kuwa maji taka yanabeba asilimia kubwa ya kemikali zinzotokana na na binaadamu wakati wa matumizi mbali mbali bila ya yeye mwenyewe kujua kuwepo uwezekano wa kupata maradhi wakati wa utumiaji wa viumbe wengine.

 
“Maji yanaburura kila kitu yanapopita pahala kama kinyesi, kemikali za viwandani, taka za kila aina na uchafu mwengine unaotokana na na binadamu na wanyama”, alisema.
 
Isamail aliwataka washiriki wa semina hiyo ambayo imejumuisha Maofisa kutoka katika taasisi za Serikali Pemba kutilia mkazo juu ya kuhifadhi mazingira hasa rasilimali za bahari na ardhi ili kuishi maisha bora na vizazi vijavyo.
 
Semina hiyo ya siku mbili ambayo ilizungumzia athari za maji taka kimazingira imetayarishwa na Afisi ya Mkemia Mkuu Zanzibar kwa kushirikiana na Idara ya Mazingira chini ya ufadhili wa Mradi wa Usimamizi wa Mazingira ya bahari ya Hindi.

No comments:

Post a Comment