BENKI ya Taifa ya Biashara NMB imetoa msaada wa vitanda na magodoro 10 yenye thamini ya 8,000,000 kwa hospitali kuu ya Mnazi Mmoja kwa lengo la kusaidi kuimarisha huduma za Afya kwa wananchi.
Akikabidhi msaada huo kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii katika Makao Makuu ya wizara hiyo, Meneje wa Benki hiyo tawi la Zanzibar Abubakar Nyangasa alisema msaada huo ni kwa ajili ya wananchi wote wa Zanzibar.
Akipokea msaada huo, kwa niaba ya Wizara na wananchi wa Zanzibar, Waziri wa Afya na Utawi wa Jamii, Sultan Mohamed Mugheiry aliishukuru benki hiyo kwa moyo wa kizalendo wa kusaidia sekta mbali mbali za huduma za jamii ikiwemo sekta ya Afya.
Alisema muda mfupi tangu tawio hilo lifungue afisi zake Zanzibar, benki hiyo imeonyesha nia yake ya dhati kwa wananchi wa Zanzibar katika kusaidiana na serikali kuimarisha huduma za jamii.
Alisema katika kipindi hicho kifupi, NMB imesaidia sekta mbali mbali ikiwemo sekta ya Elimu, Afya na Michezo, ambapo aliuelezea uamuzi wa Benki hiyo kuwa ni ushahidi wa dhati kwamba inashirikiana na serikali kuimarisha afya na huduma kwa jamii ya Wazanzibari.
No comments:
Post a Comment