Tuesday, 20 April 2010

Uvuvi watorosha wanafunzi Chambani, Mtangani

Na Suleiman Rashid, Pemba.
ZAIDI ya watoto 300 wa vijiji mbali mbali vya Chambani na Mtangani kisiwani Pemba, wameacha skuli huku 70 wakiacha kutokana na kutokana na wazazi wao kukosa taaluma juu ya umuhimu wa elimu.

Mwalimu, Salimu Ali Mohamed alieleza hayo wakati alipokuwa akisoma risala ya jumuia maendeleo CHUMATO wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya siku mbili ya kuijengea uwezo jumuia hiyo, iliyofanyika katika ukumbi wa skuli ya sekondari ya Chambani

Alisema, kwa mujibu wa utafiti mdogo uliofanywa na jumuia ya maendeleo ya CHUMATO, umegundua watoto hao hujishughulisha na shughuli za kilimo, uvuvi na vishingizio mbali mbali ikiwa pamoja na wazazi kukosa uwezo.

Risala hiyo imeeleza kuwa vijiji vya Chambani, Mtangani na Ukutini kwa kiasi kikubwa kumekuwepo na uharibifu wa mazingira unaochangia kupata mavuno hafifu ya mazao ya kilimo.
 
Mwalim Salimu, alisema maeneo mengi yenye mito chemchem na maziwa ambayo yalikuwa yakibubujika maji wakati wote hivi sasa yamekuwa yakikaukuka kutokana na kukatwa miti kwenye vyanzo maji.
 
Naye Makamo Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, alisema mipango iliyopo ni kushirikiana na jamii ya wananchi wa Chambani katika uhifadhi wa mazingira ambayo kwa kiasi kikubwa yamechafuliwa.
 
Alisema pia Jumuia hiyo imelenga kuondosha matatizo mbali mbali yanyoikabili jamii yakwemo ubovu wa barabara na utoro maskulini.











No comments:

Post a Comment