Thursday 1 April 2010

ZEC yapandisha presha ya Wabunge, Wawakilishi

Na Mwantanga Ame
TUME ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), imezizima ndoto za baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Wabunge waliokuwa wakijiandaa kukimbilia katika Majimbo mapya kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao.

Tamaa ya Wajumbe hao inatoweka baada ya baadhi yao kuanza kuikodolea macho ZEC kuona ilikuwa na mpango wa kuyavuruga majimbo yaliopo sasa.

Kuwapo kwa tetesi hizo baadhi ya Wajumbe wakongwe wa nafasi hizo walionekana kuhaha kuanza kujiimarisha katika maeneo yao ambapo ZEC imebainisha kuwa haitakata jimbo hata moja.

Majimbo yaliokuwa yakidaiwa kuwepo kwa mpango huo ni pamoja na la Mpendae, Kitope kwa Unguja ambapo mengine yapo upande wa Pemba.

Mkurugenzi wa Uchaguzi Zanzibar, Salum Kassim Ali alithibitisha kuwapo kwa taarifa hizo ambapo amekuwa mara kadhaa akiulizwa na baadhi ya Wajumbe wa Baraza hilo na Wabunge waliopo.

Alisema Tume hiyo haina mpango wowote wa kufanya mabadiko ya Majimbo yaliopo sasa kwa na yaliopo yataenda kama yalivyo katika uchaguzi Mkuu ujao.

“Nilishasema hapo awali na hivi sasa kuwa majimbo hayatakatwa katika uchaguzi Mkuu ujao bado Tume inaendelea na msimamo wake huo” alisema Mkurugenzi huyo.

No comments:

Post a Comment