Wednesday 14 April 2010

ZEC kuchunguza sababu za kuzorota uandikishaji uchaguzi mkuu

Mwanajuma Abdi
 
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Tume hiyo, Salum Kassim Ali wakati akiwasilisha mada ya muundo wa Tume na jukumu lake katika kuendesha uchaguzi Mkuu, kwenye semina ya siku moja ya kuhamasisha wanawake kushiriki katika uchaguzi.
 
Hata hivyo, alisema uchunguzi huo utakaofanywa na kampuni ya kujitegema utafanyika baada ya kukamilika awamu ya pili ya zoezi la uandikishaji kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

Semina hiyo iliandaliwa na ZEC kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP), na kuwashirikisha wadau mbali mbali kutoka asasi za wanawake Unguja na Pemba.
 
Kwa mjibu wa Mkurugenzi huyo, kitakachozingatiwa katika uchunguzi huo ni kuzorota kwa zoezi la uandikishaji ikilinganishwa na uchaguzi wa 2005, ambapo waliojitokeza walikuwa wengi.
 
Aidha, alibainisha kuwa hata wanawake wenye kawaida ya kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi kama hilo, idadi yao imepungua ikilinganishwa na chaguzi zilizopita.
 
Alikiri kuwa ZEC inakabiliwa na changamoto kubwa kuhusu hali hiyo, ingawa kwa tathmini za juujuu imebainika hali hiyo imetokana na wananchi kuchoshwa na siasa za chaguzi za Zanzibar za wakati wa kupiga kura, ambapo wanawake nao wameona hakuna haja ya kujiandikisha.

Aidha, alisema ZEC imeagiza vifaa vya uchaguzi mapema kuliko ilivyo kwa chaguzi zilizopita, ambapo watu wenye mahitaji maalum wamezingatiwa ikiwemo walemavu wasioona kwa kuwepo karatasi za kuwatambua wagombea.

Mkurugenzi huyo aliwashauri wanawake kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za uongozi katika gazi za udiwani, uwakilisi, ubunge na hata urais.

Alisema hivi sasa kuna mwamko mkubwa wa wanawake, ambao wengi wao wameonesha nia ya kugombea katika majimbo, hivyo alivishauri vyama vya siasa kuwapa nafasi akinamama wakati watakapofanya chaguzi ndogo za ndani ya vyama kuwapitisha wagombea kwa ajili ya kusimama katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

TUME ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), imesema itafanya uchunguzi kutathmini zoezi la uandikishaji wapiga kura uchaguzi mkuu ujao kutokana na idadi ndogo ya waliojitokeza.

No comments:

Post a Comment