Saturday 10 April 2010

'Kukosekana vifaa maabara huchangia kuingizwa mafuta duni'

Na Mwanajuma Abdi
 
Akizungumza na gazeti hili, Mkurugenzi wa Nishati na Madini, Omar Zubeir, alisema Zanzibar hakuna maabara yenye vifaa vya kiutaalamu vya kuchunguza bidhaa hizo, ambapo kigezo kikubwa kinachofuatwa ni makisio yanayotokana na nyaraka za kusafirishia mizigo zilizoletwa kuwa yapo katika kiwango bora kwa matumizi ya vyombo.
 
Hayo yamebainika baada ya gazeti hili kuzungumza na madereva mbali mbali wanaoendesha vyombo vya moto kulalamikia mafuta yanayoingizwa nchini kuwa chini ya kiwango.

Mkurugenzi alifafanua kuwaTanzania bara wanayo maabara ya kuchunguzia bidhaa hiyo kupitia Shirika la Viwango (TBS), ambapo wafanyabiashara wanaoingiza mafuta chini ya kiwango huchukuliwa hatua lakini Zanzibar hilo halipo.
 
Alisema lakini kwa Zanzibar bado hawajaweka maabara hiyo, kutokana na ukosefu wa fedha, ambapo mwaka 2003 -2004 walitaka kwenda kuchunguza bidhaa hiyo Tanzania Bara lakini walishindwa kufanya hivyo kutokana na bei kubwa kubwa kwani lita moja ilikuwa ni shilingi milioni 26 kwa wakati huo na kwasasa itakuwa imepanda zaidi.
 
"Maabara inahitaji fedha nyingi , ambapo kutokana na uwezo wa Serikali bado haijaweza kumudu gharama za kuweka maabara ya kuchunguzia bidhaa ya mafuta inayoingizwa nchini badala yake wanafuata alama zinazowekwa wakati wa kuingizwa bidhaa hii nchini 'Bill of Lead', alieleza Zubeir.

Aidha alifahamisha kuwa, wameamua kuwasomesha wafanyakazi wao, sambamba na kuwaajiri wataalamu ili kudhibiti hali hiyo kwa vile hivi sasa wanaangalia kwa macho, lakini hakuna vipimo vya kuthibitisha hilo.

 
UKOSEFU wa vifaa vya kuchunguzia ubora wa mafuta ya Petroli, Dizeli na mafuta ya taa unachangia kuingizwa bidhaa hizo zilizo chini ya kiwango.

No comments:

Post a Comment