UTARATIBU wa kujiunga na Vyuo Vikuu vya elimu ya juu nchini umebadilika na utaanza kutumika mwaka huu wa masomo 2010/2011.
Kwa mujibu wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), waombaji watatakiwa kuomba udahili moja kwa moja kupitia TCU kwa kutumia mtandao wa intaneti na simu za mkononi.
Utaratibu huo mpya unafuta ule wa zamani ambapo wanafunzi walikuwa wakituma maombi moja kwa moja vyuo vikuu.
Hata hivyo, utaratibu huo hautatumika kwa Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU) kilichopo Tunguu, Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Zanzibar Chukwani na Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro kwa kuwa havijajiunga na mfumo huo.
Wanafunzi wanaomba katika Vyuo hivyo, watalazimika kutumia mfumo wa zamani wa kutuma maombi yao moja kwa moja chuoni.
Utaratibu huo mpya unawahusu wale watakaoomba udahili kwa kutumia sifa za kidatu cha sita , walizozipata kuanziwa mwaka 1988 hadi mwaka 2010 na wale wenye vyeti vya nchi nyegine.
TCU imesema maombi kwa wanafunzi waliomaliza kidatu cha sita mwaka 1988 hadi mwaka uliopita na wale wenye vyeti vya nje yameanza tokea Aprili 8 mwaka huu.
Aidha Tume hiyo imesema kwa wale waliomaliza kidatu cha sita mwaka huu wataanza kuomba udahili Aprili 30 au wakati wowote majibu yao ta mitihani itakapotangazwa.
No comments:
Post a Comment