Tuesday 20 April 2010

'Jitokezeni mjiunge mfuko bima ya afya'

MFUKO wa Bima ya Afya Tanzania umewataka Maafisa na wapiganaji wa jeshi la polisi na uhamiaji hapa Zanzibar kujitokeza kujiunga na mfuko huo ili kuweza kupata huduma bora ya afya.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa kanda ya Mashariki ya Mfuko huo, Rose Ongara wakati alipokuwa akitoa mada katika warsha maalum iliyohusu mfuko huo iliyofanyika Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Muembe Madema.

Ongara alisema kwa sasa askari hao hawana budi kujitokeza kujiunga na mfuko huo kwa lengo la kuweza kupata huduma bora ya afya pindi watapouguliwa ama kuugua kwa vile mwanachama binafsi hupatiwa matibabu kutokana na fedha za mfuko huo.

Alisema bila ya kuwa mwanachama wa mfuko huo, askari hao wanaweza kupata shida pindi watapokuwa wamepatwa na maradhi kwani, alisema kwa sasa gharama za huduma ya zimepanda kwa kiasi kikubwa jambo ambalo linaweza kuwapa usumbufu.

Aidha akitoa ufafanuzi kuhusu mafanikio waliyoyapata ndani ya mfuko kwa kipndi kifupi tangu kuanzisha mwaka 1999, na kuanza kazi zake rasmi mwaka 2001,alisema kwa kiasi mfuko huo umefikia mafanikio mazuri .

Miongoni mwa mafanikio yaliyofikiwa, alisema Mkurugenzi huyo ni kuimarika kwa huduma za afya kwa wanachama na mfuko kutoa huduma kutokana na kuimarika kwa kukuza rasili mali na kuendeleza kutoa elimu kuhusu dhana ya mfuko wa afya na kuweza kueleweka zaidi.

Alisema licha ya kuwa wamepiga hatua kimafanikio bali pia mfuko huo umekuwa ukikabiliwa na changamoto ambazo zinakatisha tamaa kwa wanachama,na akazitaka chanagamoto hizo kuwa uhaba wa dawa katika vituo walivyotiliana mikataba na ukosefu wa wataalamu wa kutosha.

Hata hivyo, alisema jitihada zoinafanyika kuuzitafutia ufumbuzi ili wanachama waweze wkupatiwa huduma ziunazolingana na malipo yao na zenye kukidhi mahitaji.

Nao maafisa na wapiganaji wa polisi na uhamiaji walioshiriki warsha hiyo waliahidi kutoa ushirikiaono katika sula la kuharakisha kujiunga ili waweze kufaidika na huduma bora ya afya kwao na femilia zao.

Warsha hiyo maalumu ilihudhuriwa na wataalamu mbali mbali kutoka Mfuko huo akiwemo Mkurugenzi huyo wakanda ya Mashariki,Mkurugenzi Mkuu Emmanuel Humba,upande wa polisi ulihudhuriwa na Kamishna wa Polisi Zanzibar Khamis Simba,Kamishna Msaidizi Gabriel Simiono kutoka kitengo cha malipo na mafao Dare-es-Salam na maafisa weengine.

No comments:

Post a Comment