Monday, 10 January 2011

DK. FAUSTINE KUUKABILI MGOGORO KIBURUNGWA

Dk. Faustine kuukabili mgogoro Kiburugwa

Na Kunze Muswanyama, Dar es Salaam
 Jumanna 11, Januari 2011

WANANCHI wanaodhaniwa kuwa ni wanachama wa CCM na CUF wamesabisha vurugu huku Kiburugwa Manispaa ya Temeke wakigombea mradi wa maji uliojengwa na Benki ya dunia mwaka 2003.

Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile akiambatana na polisi alilazimika kuingilia kati kuwatuliza wananchi hao waliokuwa na jazba, ambapo tayari walikwisha vunja uzio unaozunguka eneo la mradi.

Mbunge huyo aliwataka wananchi hao kutokuwa na jazba kwani huku akizungumza kwa hekima kubwa hali iliyowafanya mashabiki wa CUF kutuliza munkari na kuanza kusikiliza wasia wa kiongozi huyo.

Alisema suluhisho na mradi huo litapatikana huku akiahidi kwenda kwa Mkurugenzi wa Manispaa, ili ibainishwe wazi na kuondosha mgogoro huo.

Chanzo cha kutoelewana kwa wananchi hao ni kufuatia mradi huo kujengwe kwenye eneo linalomikiwa na CCM, huku viongozi wa chama hicho wakishindwa kuupatia suluhisho hadi kutaka kusabisha amani.

Katika hatua nyingine, wakaazi hao wamelalamikia kitendo cha CCM kutumia huduma ya umeme inayotolewa na Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) pasipo uhalali wowote katika eneo hilo linalozunguka ofisi hiyo ya CCM na mradi huo wa maji.

Wakizungumza na waandishi wa habari katika eneo hilo, wakazi hao walisema wanashangaa kulipishwa kila siku shilingi 2,500 za umeme ilhali pesa hizo zikiingia mifukoni mwa wajanja wachache na kulisababishia Shirika hilo hasara kubwa.

Walidai kuwa hadi sasa ccm katika eneo hilo wanadaiwa kiasi cha shilingi milioni 36 zikiwa ni bili ya umeme jambo linalofanya kuwa na uwezekano mkubwa wa kukatiwa umeme muda wowote na kuweka uwezekano wa kukosa kabisa huduma hiyo.

No comments:

Post a Comment