Friday 14 January 2011

KIKWETE AZUNGUMZA NA MJUMBE WA RAIS KIBAKI.

Kikwete azungumza na mjumbe maalum wa rais Kibaki


Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete jana alikutana na kufanya mazungumzo na mjumbe maalum wa Rais Mwai Kibaki wa Kenya.

Katika mkutano uliofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, mjumbe huyo maalum, Robinson Njeru Githae ambaye ni Waziri wa Maendeleo ya Jiji la Nairobi, amemkabidhi Rais Kikwete ujumbe maalum kutoka kwa Rais Kibaki.

Katika mazungumzo yao, Rais Kikwete na Waziri Githae wamezungumzia maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili na jinsi ya kuboresha uhusiano huo.

Viongozi hao pia wamejadili maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na changamoto zinazoikabili Jumuia hiyo na jinsi Tanzania na kenya zinavyoweza kuchangia katika kuboresha mchakato wa kuongeza mshikamano baina ya nchi wanachama wa Jumuiya hiyo. Nchi wanachama wa EAC ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

No comments:

Post a Comment