Mwakilishi awataka wataalamu wa maabara kutunza siri
Ali Mohamed, Maelezo
Jumanne 11, Januari 2011
MWAKILISHI jimbo la Mpendae, Mohamed Said Mohamed amesema kuna umuhimu mkubwa kwa maabara za Afya kutunza siri za wagonjwa wanaopima afya ya zao.
Akizungumza na wafanyakazi wa maabara wakati akifungua semina ya siku mbili ya wafanyazi wa maabara za hospiltali binafsi za Unguja huko Lumumba, alisema wataalamu wa maabara ndio wanaofahamu kwa kina matatizo ya Afya za wagonjwa.
Alisema maabara ni chombo muhimu katika kutafuta chanzo cha ugonjwa unaowakabili wanaadamu hivi watumishi lazima wafuate maadili ya kazi zao kwa kutowaeleza wasiohusika yale waliyoyabaini wakati walipowapima.
Mwakilishi huyo, alisema maabara zina umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya afya za wananchi na akawashauri wataalamu katika sekta hiyo kuzingatia umuhimu huo wanapotoa huduma kwa jamii.
Alisema kulinda maadili ya kazi hiyo ni pamoja na kuficha siri za wagonjwa na wale ambao mgonjwa mwenyewe ataamua wafuatilie matatizo yake .
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wataalamu wa maabara Zanzibar, Asha Ahmed Othman alisema lengo la jumuiya hiyo katika awamu ya kwanza ni kuwapatia mafunzo wanachama wake wasiopungua 80 kuwandaa kuwa utoaji wa hudujma bora zaidi wateja wao.
Alisema pamoja na kutoa mafunzo hayo pia watazikagua maabara zote za hospitali binafsi ili kuangalia ubora wa huduma za maabara hizo na zitakazo gundulika kuwa na mapungufu itawataka wamiliki wake kuziboresha ziweze kutoa huduma nzuri na za haraka kila inapohitajika.
Mapema Katibu Mtendaji wa jumuiya hiyo, Mwinyi Mselem alisema jumuiya hiyo iliyoanzishwa mwaka 2002 na kwa sasa inawachama 182 ambapo mwanzilishi wake ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kabla ya kuwa Rais
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment