Friday 14 January 2011

HOFU YA KIYAMA YALIKUMBA JIJI LA DAR - ES - SALAAM

Hofu ya kiyama yalikumba jiji la Dar es Salaam

Vipeperushi vyaanisha mwisho wa dunia
Sheikh, Mchungaji wawatoa hofu wananchi
Na Kunze Mswanyama,Dar

HOFU na wasiwasi imetanda miongoni mwa wakaazi wa jiji la Dar es Salaam, baada ya kusambazwa vipeperushi vinavyoelezea kuwa mwisho wa dunia ni Mei 21 mwaka huu.

Vipeperushi hivyo vimezagaa sehemu mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam ambapo watu waliovisambaza hawajulikani, ambavyo vimezua hofu hofu miongoni mwa wananchi huku hatma yao wakiielekeza kwa Mwenyezi Mungu.

Katika jiji la Dar es Salaam jana wananchi wengi walikuwa kwenye makundi makundi wakijadiliana hali itakavyokuwa siku hiyo ya Mei 21, ambapo ndipo itakuwa kiyama.

Wakisimulia kadhia hiyo, wananchi waliozungumza na gazeti hili, walisema tukio la kubashiri siku ya mwisho wa dunia halijapata kutokea watu.

Vipeperushi hivyo vilivyokuwa na kichwa cha habari kisemacho, ‘Mwisho wa Ulimwengu Umekaribia, Mungu Mtakatifu Ataleta Siku ya Hukumu Mei 21,2011", kilifanya baadhi ya watu kwenda kuwahoji viongozi wao wa dini kwa kukaa kimya na kutosema lolote juu tukio hilo la kutisha.

Katika vipeperushi hivyo zimenukulia baadhi aya kitabu cha bibilia, ikiwaamuru watu wote kuacha maovu na kumrudia Mwenyezi Mungu ili kujiokoa na hukumu hiyo ijayo ya kutisha iyakayotokea mwezi Mei mwaka huu.

“Wale wote wasiokuwa tayari katika maandalizi yao watatumbukia katika hukumu hiyo kuu na ya kuitisha ambayo haijawahi kutokea na kuwa hakimu wake ni Mwenyezi Mungu na kwa kawaida yake hapokei wala kutoa rushwa na tena hapendelei mtu yoyote, hivyo kuwa hakimu wa haki tena kwa wote”, vilieleza vipeperushi hivyo.

Sheikh wa Msikiti wa Kigamboni jijini Dar es Salaam, Nassor Bin Hassan Maulid, alisema yeye kamwe haamini kama kweli Mei 21 itakuwa ndiyo mwisho wa dunia na kusimama kwa kiyama.

"Huo ni uzushi tu na hao watu hawana lolote ni matapeli tu wanaotumika kuwatia hofu na kuwaogopesha watu", alisema Sheikh huyo.

Sheikh Maulid, alisema hakuna mtu anayejua siku ya kiyama na kuwataka watu waondoe hofu ya vitisho hivyo.

Naye Mchungaji Philimon Patric wa Kanisa la Wasabato, Kurasini alisema hakuna ajuaye saa wala siku ya kuja kwa Bwana, kwa kuwa yeye pekee ndiye anajua lini na saa ngapi atakuja kutoa kuhukumu ulimwenguni.

Kwa muda mrefu sasa hapa jijini Dar es sana kumekuwa na watu wanaosambaza vipeperushi wa uzushi kwa kutumia mbinu mbali mbali ikiwemo vipaza sauti wakisema watu watubu na waache dhambi kwa kuwa hakimu wa dunia iko karibu.

No comments:

Post a Comment