Monday, 9 May 2011

BASRA YAILAZA NYUNDO 4-0

Basra yailaza Nyundo 4-0

Na Hilal Haji, MCC
TIMU ya soka ya Nyundo FC imetandikwa magoli 4 - 0 na Basra FC katika mchezo wa ligi daraja la pili wilaya ya Micheweni, uliochezwa katika kiwanja cha Wingwi Mapofu.
Basra ilionekana kuutawala mchezo huo kwa kiasi kikubwa na kuweza kutoa burdani safi kwa mashabiki wake waliofika kiwanjani hapo.
Magoli ya Basra yalifungwa na Khamis Amour na Vuai Serengo.
Katika mchezo mwengine uliochezwa katika kiwanja cha Kiembesamaki, timu ya Kibweni iliweza kuadhibiwa kwa goli 1 - 0 na FC Lion ikiwa ni ligi daraja la pili wilaya ya Magharibi Unguja.

No comments:

Post a Comment