Monday, 9 May 2011

LIGI KUSINI YAPAMBA MOTO

Ligi Kusini yapamba moto

Na Ameir Khalid
TIMU ya soka ya Mapinduzi ya Jambiani imeifunga Paje Star ya Paje magoli 4 - 1, katika mchezo wa ligi daraja la pili uliovurumishwa kwenye kiwanja cha Sungusungu Jambiani.
Katika mchezo wa ligi daraja la tatu, Kajengwa Stars iliwaangushia kipigo cha magoli 5-0 jirani zao wa Kiniju pia ya Kajengwa, pambano lilolochezwa kiwanja cha Mwehe Makunduchi.
Aidha, kwenye uwanja wa Kashangae Paje, Newboys ya Mtende na Bushibushi ya Jambiani, zilitoka sare ya kutofungana.

No comments:

Post a Comment