Zimamoto yaizima Bridge
Na Mwajuma Juma
TIMU ya Zimamoto imezidi kujikita kileleni mwa ligi daraja la kwanza Taifa baada ya kuilaza Bridge magoli 3-1, katika mchezo uliochezwa uwanja wa Mao Dzedong.
Kwa ushindi huo, Zimamoto imeweza kufikisha pointi 16 na kutanua katika kiti cha uongozi wa ligi hiyo.
Mchezo huo ulikuwa na upinzani mkali ambapo timu zote zilijitahidi kucheza vizuri, lakini Zimamoto ndiyo iliyoonekana kuizidi ujanja Bridge na kuibuka na ushindi huo.
Zimamoto ilianza kupiga hodi kwenye lango la Bridge kunako dakika ya nne kwa goli lililofungwa na Hakim Khamis. Goli hilo lilidumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili kiliendelea kwa timu zote kufanya mashambuliaji, lakini walikuwa Zimamoto tena waliofanikiwa kuandika goli la pili lililofungwa na Khatib Said Lahe kunako dakika ya 57.
Mshambuliaji, Mohammed Suleiman, aliipaitia Zimamoto goli la tatu kunako dakika ya 87.
Goli pekee la kufutia machozi la Bridge lilifungwa na Uzia Abdalla kunako dakika ya 73 .
Katika mchezo mwengine uliochezwa uwanja wa Fuoni, JKU iliitafuna Mlandege kwa magoli 3-0.
Mgoli ya JKU yalifungwa na Amiri Kimbwini, Ali Kaka na Is-haka Othman.
JKU na Bridge sasa zinashika nafasi ya tisa zikiwa na pointi kila timu zikitofautiana kwenye magoli ya kufunga na kufungwa.
Monday, 9 May 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment