Friday, 6 May 2011

WAANDISHI WATAKIWA KUUFANYIA TATHMINI MICHANGO KUILETEA NCHI MAENDELEO.

Waandishi watakiwa wafaufanyie tathmini mchango kuiletea nchi maendeleo

Na Zuwena Shaaban, Pemba
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Dadi Faki Dadi amesema ipo haja ya waandishi wa habari kukaa na kujithamini mchango wao katika kuiletea nchi kimaendeleo.
Dadi alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko katika ukumbi wa TASSAF, Chake-Chake wakati wa maadhimisho wa uhuru wa habari zilizofanyika katika ukumbi huo hapa Kisiwani Pemba.
Alisema waandishi wa habari ni watu muhimu sana katika ulimwengu ambao unahitaji kupata habari ambazo ni za kweli kwani dhima kubwa ya waandishi kuweza kuchanganua na kuitangaza dhima ya utawala bora na kuleta maendeleo ya kweli nchini.
Alieleza kuwa waandishi waitumie nafasi waliyonayo kitaalamu kabisa katika kuelimisha jamii na kuweza kukosoa pale ambapo palikosewa, lakini katika ukosoaji huo lazima wapime katika kujenga na kuweza kuzidisha amani iliyopo.
“Tafuteni habari kadri vile taaluma yenu ilivyowaelekeza ila tambueni kwamba taarifa nyengine mpaka ungiye ndani kabisa katika kutafuta ukweli kwani utakapoegemea upande mmoja tu basi lazima malumbano yatatokea na sisi hatutaki yafikie hayo”,alisema Mkuu huyo.
Alifafanuwa kuwa kwa sasa taarifa sio ngumu kuzipata kwa vile watu wengi wanauelewa dhana ya utawala bora na huku tukiwa katika serikali hii ya awamu ya saba ikiwa na mfumo wa Kitaifa na kuona kuwa viongozi wote waliyo katika Serikali hii wanawajibu kulinda tofauti zao za chama wakiweko makazini kwa kuweza kushirikiana katika kutatua kero za wananchi na kuwajengea mazingira boara.
Aidha alisema serikali ina mpango wa kuwawezesha waaandishi wote wawe sawa katika kuitetea jamii juu ya masuala mbali mbali ambayo huibua mijadala mizito kwa wahusika na kuweza kupata ufumbuzi wa kweli kweli.
Alifafanua kuwa katika kuadhimisha siku ya uhuru wa habari duniani hii isiwe tu kupeana zawadi pia iwe ni darasa tosha la kuweza kuchanganua changamoto mbali mbali ambazo zilizowakumba waandishi katika kipindi cha mwaka mzima na kujitathmini.
Naye Mwenyekiti wa Pemba Press Club Khatib Juma Mjaja alisema kuwa kifungu 59 wa mkataba wa Kimataifa ni haki kila mmoja kupata habari kwa hiyo jamii ielewa kuwa waandishi wako katika kuitetea jamii katika kufikia malengo bora pamoja na kuataka kuimarisha dhana mzima ya utawala bora katika kazi kwani bila ya kujua viongozi wanafanya nini basi viongozi hao watakaa bila ya kufuata dhima mzima ya utawala bora.
Alisema Pemba Press Club (PPC) Kisiwani Pemba itahakikisha waandishi wote Kisiwani humo kuwa ni waandishi wa kweli na wenye kuibua taarifa sahihi ambazo jamii inataka kuelewa na sio kukaa tu huku jamii ikiwa inajiinamia kwa simazi za changamoto ambazo zinawakabili bila ya kupatiwa ufumbuzi.
Katika kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari nchini Mwenyekiti huyo alisema ipo haja ya waandishi wa habari kuthaminiwa na kuweza kupewa habari ambazo ni zakweli na uhakika bila ya watumishi wa Serikali hii kuogopa kusema ukweli kwani ile lengo la kuwapasha wananchi na kuandika ukweli liweze kupatika.
Maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo Mei 3, na hapa kisiwani Pemba sherehe hizo zilifana zikiwa zinasimamiwa na Pemba Press Club na kuweza kuhudhuriwa na waandishi wote kisiwani pemba.

No comments:

Post a Comment