Monday, 9 May 2011

KIBWENI YAPATA USHINDI

Kibweni yapata ushindi mwembamba

Na Rahma Suleiman, MCC,
TIMU ya Kibweni imepata ushindi baada ya kuilaza timu ya Halmashauri ya wilaya ya Magharib goli kwenye mchezo wa ligi daraja la pili.
Mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa bubu ulianza taratibu huku kila timu ikicheza kwa tahadhari na kumaliza dakika 45 za kwanza zikiwa hakuna mbabe.
Kibweni iliandika goli hilo pekee kunako dakika ya 81 lililofungwa na Shamsi Mohammed.
Kwa matokeo hayo, Kibweni imefikisha pointi 13 huku Halmashauri ikiwa na pointi 17.

No comments:

Post a Comment