Friday, 6 May 2011

ASKOFO ABAINISHA CHANGAMOTO YA KUONDOA UMASIKINI.

Askofu abainisha changamoto ya kuondokana na umasikini
Na Nalengo Daniel, Morogoro
ASKOFU Kiongozi wa Kanisa la Moravian Tanzania Alinikisa Cheyo amesema kuwa endapo kila mwananchi atajishughulisha na shughuli za kujiletea maendeleo na kuondokana na utegemezi ni dhahiri taifa litaondokana na umasikini.
Askofu huyo aliwataka wananchi kuacha tabia ya kuitegemea serikali pekee, na kwamba haiwezi kuleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja, na badala yake wafanyekazi zenye kuwaletea manufaa ambazo zitasaidia kuinua kipato chao na uchumi nchini.
Kauli hiyo aliitoa mjini hapa wakati akifungua semina ya siku sita katika kanisa la Moravian Morogoro lililopo eneo la kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro ikiwa na lengo la kufundisha kujitegemea kiuchumi, kiroho na kujitunza ili kuwa na afya nzuri.
Alisema kuwa idadi kubwa ya wananchi ni tegemezi na kuwataka kuacha tabia hiyo, na kwamba mtu akijitegemea kiuchumi, kanisa pia litajitegemea na nchi itaondokana na umasikini na kwamba kujishighulisha ni sehemu ya kiroho.
“Watanzania ni wepesi wa kuridhika hawataki kujibidiisha, ikitokea ndugu yao mmoja ana kipato kizuri wote wanamtegemea yeye pekee bila kujishughulisha tabia hiyo syo nzuri kiroho na kiafya.
Aidha alizungumzia suala la kujitunza kiafya ambapo alisema kuwa uchafu wa mwilini ni dalili ya uchafu wa rohoni, na kwamba ikiwa mkristu atashindwa kuishi maisha ya kawaida hata ya rohoni yatamshinda.
Aliwataka wakristo kuishi maisha ya rohoni, na kutomdharau mtu kutokana na imani yake, na kwamba imani katika kirsto hairuhusu kufanya hivyo.No comments:

Post a Comment