Monday, 20 June 2011

AFRIKA YAKARIBIA KUPATA WAWAKILISHI OLIMPIKI

Afrika yakaribia kupata wawakilishi Olimpiki

CAIRO, Misri
TIMU nane zitakazocheza mashindano madogo mwezi Disemba kutafuta nchi tatu za kuiwakilisha Afrika kwenye michuano ya Olimpiki mwaka 2012, zinakaribia kutimia.
Morocco, Algeria na Misri kutoka Afrika Kaskazini, zimekata tiketi zao katika ngarambe hizo za Disemba baada ya michezo yao mwishoni mwa wiki iliyopita.
Aidha Senegal, Ivory Coast na Nigeria zimetinga hatua hiyo, huku Mali ikitumai kuungana nazo, wakati Afrika Kusini ikiwa nchi pekee kutoka kusini mwa bara la Afrika kushiriki patashika hiyo.
Michuano hiyo inayotarajiwa kufanyika Disemba 2 hadi 18, itaamua timu tatu zitakazopeperusha bendera ya Afrika katika Olimpiki ya majira ya kiangazi jijini London, huku timu ya nne ikicheza mchezo wa kuamua dhidi ya timu kutoka bara la Asia.

No comments:

Post a Comment