Friday 17 June 2011

MFUKO FRDHA ZA MUUNGANO KUAZA MWAKA HUU.

Mfuko fedha za Muungano kuanza mwaka huu
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri wa Muungano Tanzania, Mizengo Peter Pinda amesema mfuko wa pamoja wa hazina baina ya Serikali Mapinduzi Zanzibar na serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania unatarajiwa kuanza mwaka huu.
Pinda aliyasema hayo jana, Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu masuali la papo kwa papo kutoka kwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alisema mfuko wa pamoja utakuwa tayari kabla ya kumalizika kwa mwaka huu, ambapo utaziwezesha SMZ na SMT kutumia pamoja kwa mujibu wa katiba ya Tanzania.
Alieleza Wabunge hao kwamba tayari Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeshapeleka mapendekezo yake katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo taratibu zinaendelea kufanyika na baada ya kukamilika utaanzishwa rasmi.
Aidha akitoa ufafanuzi kuhusu mjadala wa posho unaoendelea katika Bunge hilo, ambalo suala hilo aliliuliza Mohammed Habib Mnyaa alihoji kama posho zinazolipwa kwa mujibu wa katiba ya nchi zinauwezo wa kuondolewa kiholela.
Waziri Mkuu Pinda alifafanua kuwa zipo posho zimewekwa kwa mujibu wa sheria ambazo haziwezi kuondolewa kiholela kwa vile zimo katika katiba.
Alisema kuna posho ambazo Spika anaweza kuziomba kupata idhini kwa Rais kwa ajili ya kuwalipa wabunge kutokana na kazi zinazofanywa.
Alifahamisha kuwa, kuna posho ambazo watu wanastahiki kulipwa kwa mujibu wa kufanya kazi kupita masaa ya kawaida.
Waziri Mkuu Pinda alimshauri Mbunge Zitto Kabwe ambae ameanzisha mjadala huo na kuufanya ni msimamo wa CHADEMA, ambapo aliwaeleza ni bora mtu aziache posho hizo yeye binafsi na kuagiza ni bora wakaziache ziingie katika mfuko wa Hazina.
Aliendelea kutoa mfano madiwani hawana mishahara isipokuwa wanalipwa posho, hivyo posho zikiondoshwa hao watafanywa kitu gani.
Alimueleza Spika kwamba ni busara posho za wabunge zikaingizwa katika mishahara yao ili ziwasaidia kwani wanakazi kubwa, ambapo posho hizo zinawasaidia kuwapa wananchi kwani wanapotoka katika Bungeni watu wanakamata masharti wanawaomba nauli.

No comments:

Post a Comment