Zanzibar yatamba UMISETA
Na Donisya Thomas
KITIMTIM cha michezo ya Umiseta inayoshirikisha skuli za sekondari nchini Tanzania, inazidi kupamba moto Wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa kiongozi wa msafara wa wanamichezo wa Zanzibar Mussa Abdulrabbi, timu za Zanzibar zimeweza kuanza vizuri mashindano hayo na kutoa matumaini ya kurudi na vikombe.
Alisema kwa upande wa mchezo wa mpira wa miguu, Zanzibar ilifanikiwa kuilaza timu ya Kanda ya Magharibi kwa mabao 2-0.
Aidha Abdurabbi ambae pia ni Katibu wa Chama cha Mpira wa Mikono Zanzibar (ZAHA), alisema katika michuano ya mpira wa mikono, Zanzibar pia iliibuka kidedea kwa kuichapa Dar es Salaam mabao 26-11.
Hata hivyo, kwa upande wa netiboli, mabanati wa Zanzibar wameshindwa kuwatambia mahaloo wa jiji la Dar es Salaam baada ya kukubali kipigo cha mabao 25-22.
Aidha kiongozi huyo wa msafara wa Zanzibar alizidi kuliambia gazeti hili kwamba katika mchezo wa mpira wa wavu kwa wanawake, Zanzibar iliifungia kazi Kanda ya Kati kwa kuipa kipigo cha seti 3-0.
Friday, 17 June 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment