Friday 10 June 2011

WAFANYAKAZI KILIMO USHIRIKA WAIKIMBIA OFISI

Wafanyakazi kilimo, ushirika waikimbia ofisi

 Ni baada ya jengo kutaka kuporomoka
Na Mwanajuma Abdi
ZAIDI ya wafanyakazi 100 wa Idara ya Kilimo na Idara ya Vyama vya Ushirika jana walikubwa na hofu kubwa huku walikimbizana ovyo katika ngazi, baada ya jengo kudata katika eneo la Forodhani mjini hapa.
Mkasa huo ulitokea jana, baina ya saa 5:55 na 6 machana, huku ambapo wafanyakazi hao wakikimbia kutaka kuokoa maisha yao kwa kuogopa kuangukiwa na jengo hilo lililo katika hifadhi ya Mji Mkongwe.
Wakizungumza na gazeti hili, wafanyakazi hao walisema jengo hilo la ghorofa mbili ambalo linajumuisha Idara mbili za wizara ya Kilimo na Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wananchi Kiuchumi na Ushirika.
Walieleza jengo hilo lilianza kudata katika ghoroga ya pili na kuendelea na mtikisiko ghorofa ya kwanza hali iliyowafanya wapate hofu ya maisha yao na kusababisha kukimbilia nje.
Walifahamisha kuwa, Mamlaka ya Mji Mkongwe juzi ilifika katika jengo hilo kwa ajili ya kulikaguwa na kufanya tathmini lakini ndipo jana lilipodata.
Hata hivyo, walisema viongozi wa Idara hizo waliwaambia wafanyakazi hao wasiingie katika ofisi hizo, jambo ambalo wamelazimika kubakia nje kwa muda wote hadi hapo watakapopata maelekezo kutoka kwa viongozi wao.
Walifafanua kuwa, jengo hilo ni bovu kwa muda mrefu ambapo kipindi cha mvua linavunjisha maji kama muembe, ambapo baadhi ya mipasuko na mwani uliosababishwa na maji ya mvua waliwaonyesha waandishi wa gazeti hili.
Walisema jengo hilo halifai kwa matumizi ya binaadamu kwa sasa kwa vile limeshaboba maji kutokana na maumbile yake limejengwa kwa udongo, chokaa na mawe, ambalo ni la tangu enzi na enzi.
Jengo hilo linajumuisha wafanyakazi wa Idara ya Kilimo 85 na Idara ya Vyama vya Ushirika 45, ambapo wakati lilipodata Mkurugenzi Khamis Daudi Simba alikuwepo, ambae nae aliungana na wafanyakazi kukimbilia nje na kuwaamuru wasiingie ndani kwa ajili ya usalama wao.
Katibu wa Kilimo na Maliasili, Affan Maalim alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo alisema serikali inaendelea kuwatafutia eneo mbadala la ofisi ili kunusuru maisha ya wafanyakazi.

No comments:

Post a Comment