Tuesday, 14 June 2011

DARAJA LA PILI MWENDO MDUNDO

Daraja la 2, mwendo mdundo

Na Suleiman Bangaya
LIGI soka daraja la pili taifa imeendelea katika viwanja tafauti, huku sare ikitawala.
Katika uwanja wa Dimani, maseremala wa Young Carpenters na WIPA zilitoshana nguvu kwa sare ya 1-1, wakati Strong Fire na New Power nazo zikapata sare tasa.
Nayo Bambi Kids ikaionesha cha mtema kuni timu ya Uroa kwa kuikaanga kwa magoli 2-1.
Wakati huo huo, timu ya Black Worriers ya Bweleo Wilaya ya Magharibi, imerudi upya katika medani ya soka baada ya kukaa nje ya viwanja kwa miaka mingi.

No comments:

Post a Comment