Tuesday 14 June 2011

MANYARA YAONDOKA NA MATUMAINI KIBAO.

Manyara yaondoka na matumaini kibao

Na Donisya Thomas
KOCHA Mkuu timu ya taifa Manyara Stars inayoundwa na vijana walio chni ya miaka 23, Jamhuri Kihwelo 'Julio', amesema wanakwenda Nigeria wakiwa na matumaini makubwa ya kushinda mchezo wa marudiano utakaochezwa Juni 18.
Akizungumza na Zanzibar Leo kwa njia ya simu kutoka jijini Dar es Salaam, Kihwelu amesema ushindi wa bao 1-0 walioupata katika mchezo wa kwanza Juni 6, umewazidishia nguvu na ari ya kufanya vizuri katika pambano la marudiano.
Alisema licha ya kuelewa ugumu wa mchezo huo, lakini wamejipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi mwengine na kusonga mbele ili kupata nafasi ya kushiriki katika fainali za Olimpiki kwa vijana zitakazofanyika mwaka 2012 nchini Uingereza.
Kocha huyo alisema tayari ameshawajenga kisaikolojia wachezaji wake na kuwaandaa katika hali ya ushindi, ili lengo la kucheza mashindano ya Olimpiki jijini London litimie.
"Baada ya mechi ya hapa Dar, nimewajenga vijana wangu kifizikia na kisaikolojia ili waingie uwanjani wakijiamini na kucheza kwa lengo la kushinda", alisema Julio.
Aidha alifahamisha kwamba changamoto waliyoipata kwa Mohammed Dewji imezidi kuwapa moyo wachezaji wake ambao wamemuahidi ushindi katika pambano hilo.
Aidha aliwataka Watanzania kuiombea dua timu hiyo, ili iweze kushinda katika mchezo huo na kulipandisha soka la Tanzania katika chati za juu.
Kikosi cha Manyara kinatarajiwa kundoka leo kikiwa na wachezaji 15, kikihitaji ushindi au sare ya aina yoyote kuweza kosonga mbele.

No comments:

Post a Comment