Ligi netiboli Unguja kuanza Juni 18
Na Mwajumwa Juma
LIGI ya mchezo wa netiboli kanda ya Unguja, inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 18 mwaka huu.
Patashika hiyo inayoshirikisha timu 15 zikiwemo saba za wanaume na nane za wanawake, itakuwa ikichezwa katika uwanja cha Gymkhana mjini hapa.
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Zanzibar (CHANEZA) Rahima Bakari, amesema kuwa mechi ya ufunguzi katika michuano hiyo, itazikutanisha timu ya maafande wa Polisi na Msambweni kwa upande wa wanaume.
Hata hivyo, alisema kuwa ratiba kamili ya ligi hiyo haijapangwa lakini inatarajiwa kutolewa wakati wowote kuanzia sasa.
Alisema uzinduzi huo utatanguliwa na maandamano ya timu zote 15 zitakazoshiriki maandamano hayo, yatakayoanzia nje ya uwanja.
Timu zinazoshiriki ngarambe hizo kwa upande wa wanaume, ni JKU, Msambweni, Polisi, Sogea, Jitegemee, Amani na Pangawe, huku JKU, Mafunzo, Valantia, Tuko imara, Ikulu, Zimamoto, Nyuki na Amani zitakuwa kwa wanawake.
Tuesday, 14 June 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment