Friday, 10 June 2011

ZIWANI YACHEMKA KAMISHNA CUP

Ziwani yachemka ‘Kamishna Cup’

Na Suleiman Bangaya
MASHINDANO ya michezo mbalimbali kuwania ‘Kamishna Mussa Cup’, yameendelea jana katika viwanja vya Ziwani.
Katika mchezo wa mpira wa kikapu, timu ya Sebleni iliitambia Ubago kwa kuichapa seti 2-0, huku Kiponda ikiipondelea mbali Mkwajuni kwa seti 2-0 pia.
Na katika netiboli, Muembeladu ikaonesha cha mtema kuni Mkwajuni kwa kuichakachua bila huruma kwa kipigo cha magoli 52-14.
Kwa upande wa soka, Kisauni ikilala mbele ya Muembemakumbi kwa kichapo cha mabao 3-2, wakati shehiya ya Shangani ikarambwa 3-1 na Shangani.

No comments:

Post a Comment