Friday, 17 June 2011

WASANII TANZANIA WAALIKWA MAONESHO ITALIA

Wasanii Tanzania waalikwa maonesho Italia

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WASANII wa fani mbalimbali nchini Tanzania, wametakiwa kujiandikisha kwa ajili ya kushiriki maonesho ya sanaa ya kimataifa yanayotarajiwa kufanyika mjini Rho Italia.
Taarifa zilizopatikana kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), zimefahamisha kuwa, maonesho hayo ya 16 yamepangwa kuanza Disemba 3 hadi 11, mwaka huu.
Imeelezwa kuwa, maonesho hayo yanalenga bidhaa za asili na za kiutamaduni kutoka nchi mbalimbali duniani zikiwemo za muziki, ngoma, mapambo, mavazi na vyakula ambazo kwa ujumla wake zinaelezea historia ya nchi na watu wake.
Kupitia mwaliko huo, BASAZA imevihimiza vyama na mashirikisho ya sanaa, wasanii, wadau wa sanaa kutumia fursa hiyo kuonesha kazi mbalimbali za sanaa katia tamasha hilo.
Taarifa hiyo ya BASAZA imetolewa na Katibu Mtendaji wa baraza hilo Ghonche Materego, ambaye amewataka wasanii wa Tanzania popote walipo kuchangamkia nafasi hiyo ili kujitafutia soko pamoja na kuitangaza nchi yao kupitia sanaa.
Materego amesema kwa wale watakaopenda kushiriki maonesho hayo, wanaweza kupata maelekezo zaidi kupitia tovuti : www.artigianoinfiera.it au kupiga simu + 390231911911 au faksi +390231911920.

No comments:

Post a Comment