Muhimbili waandamana
Na Kunze Mswanyama
WANAFUNZI wa Chuo Kikuuu cha Muhimbili jijini Dar es Salaam, jana waliaandamana kuishinikiza wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuondoa tangazo lililotaka kuvunjwa kwa serikali za wanafunzi na pia kuvunja cheo cha Urais katika Chuo hicho.
Wanafunzi zaidi ya 1500 na ambao walikuwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali, walikutana na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Suleiman Kova ambaye baada ya mazungumzo baina yao, aliwapa baraka zake na hivyo kukutana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Prof.Hamis Dihenga na kufanya mazungumzo ya faragha.
Mkutano huo wa dharura ambao pia ulihudhuriwa na wawakilishi wa jeshi la polisi kutoka kanda maalumu, ulihudhuriwa na wawakilishi saba wa upande wa wanafunzi ambao waliongozwa na Rais wao Gervas Shayo na Makamu wake Salim Jaribu ambao hata baada ya kutoka kwenye mkutano majira ya saa 8, walikuwa hawajakubaliana na upande wa wizara hiyo.
Akiwahutubia wanafunzi hao, Shayo aliwaambia kuwa, kimsingi hawajakubalina lakini pia wakiitaka serikali iondoe tangazo hilo ambalo hata Kova alipolisikia alikiri kuwa kuna jambo la msingi ndiyo maana katuruhusu kuingia wizarani, au siyo jamani?, alisema huku akiwauliza wanafunzi hao.
Aliendelea kusema kuwa majibu mepesi waliyopewa na katibu mkuu hayajawaliridhisha hivyo wataendelea kukaa hapo kwa kuwa ni nyumbani kwao hivyo aliwasihi wanafunzi wenzake kutokata tamaa kwa kuwa nchi nzima inawasubiri ili kuleta ukombozi kwa wanafunzi nchi nzima.
Kwa upande wake Spika wa Bunge la Chuo hicho Amir Madukenya ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa nne akisomea Udaktari, alisema tangazo hilo ambalo pia linampa madaraka makubwa mlezi wa wanafunzi.
"Uanajua baraza hii ni serikali kamili kama zilivyo nyingine inahitaji uhuru, kuaminiwa pia isiwe tegemezi hivyo kuingiliwa ni sawa na kuiingilia serikali ya Kikwete jambo ambalo si utawala bora",alisema Spika Madukenya.
Akizungumzia tangazo hilo,Madukenya ambaye aliwakilishwa na waziri wa Sheria na Katiba wa chuo hicho na ambaye ni mwanamke pekee katika serikali hiyo, Linda Saimoni,aliwaambia waandishi wa habari kuwa serikali inataka viongozi wawe na daraja la ufaulu la ngazi ya GPA 3.5 jambo ambalo ni gumu na hata kama wapo wengi wao hawataki uongozi.
Hadi mwandishi anaondoka eneo la wizara hiyo ambayo pia ipo karibu kabisa na Ikulu, kikao hicho kilikuwa kinaendelea na hata Afisa habari wa wizara hiyo Magdalena Kishiwa alipotafutwa baadae alisema kuwa bado kikao hakijaisha hivyo atatoa taarifa rasmi leo.
Mwaka 2009 serikali ilitoa tangazo kwenye gazeti la serikali ikitaka vyuo vyote vikuu kuvunja serikali zao na pia kuondoa cheo cha urais na kuingiza cha Mwenyekiti lakini pia kumpa mlezi wa wanafunzi na baraza la chuo madaraka makubwa ambapo wanaweza kuvunja serikali hiyo muda wowote ikibidi jambom linalopingwa na wanafunzi hao ambapo tayari maandamano makubwa vpia yameripotiwa mkoani Dodoma.
Monday, 13 June 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment