Monday 18 April 2011

335 WAHITIMU CHUO CHA AFYA ZANZIBAR

355 wahitimu chuo cha afya Zanzibar

Na Fatma Kassim, Maelezo


WAZIRI wa Afya, Juma Duni Haji amesema kuwa kuhitimu kwa wanafunzi 355 wa kada tofauti kutasaidia kupunguza uhaba wa wafanykazi katika mahospitali na vituo mbali mbali Unguja na Pemba.
Amesema uhaba wa watoa huduma za afya limekuwa ni tatizo kubwa hasa kisiwani Pemba ambako kuna upungufu mkubwa wa wafanyakazi wa kada tofauti ambapo wahitimu hao watasaidia kupunguza tatizo hilo kisiwani humo.
Duni ameyaeleza hayo huko Chuo cha Taaluma za Sayansi Mbweni katika mahafali ya 18 ya wahitimu wa kada Tofauti ikiwemo wauuguzi wakunga na wauguzi wa wataalamu wa afya ya akili, wauguzi wa afya ya jamii kiwango ‘B’, maafisa watabibu na maafisa watabibu wa afya ya kinywa na meno, maafisa Maabara, maafisa wa madawa na maafisa wa afya na mazingira.
Amewataka wahitimu hao kufuata sheria na taratibu na desturi za taaluma za afya kwa lengo la kutoa huduma bora watakapoanza kazi zao wakiwa mahospitalini na vituo vya afya na kuwataka wafate ushauri kwa waliowatangulia katika fani hiyo.
Alisema haitopendeza kupelekewa sifa za malalamiko ya utendaji mbovu kutokwa kwa wanaopewa huduma ambapo amesema wizara haitokubaliana na hayo na kuwataka kuwa mifano mizuri katika utendaji wao wa kazi.
Amefahamisha si lengo la Wizara ya Afya na Serikali ya Umoja wa kitaifa kwa ujumla kuyaviza bali ni changamoto inazoikabili Sekta ya afya ambapo wizara imeelekeza nguvu za pekee katika kukiimarisha Chuo hicho kwa vile ndicho kinachotoa wataalamu muhimu kwa jamii.
Katika kuimarisha huduma za chuo na za afya Chuo hicho kitajitahidi kuchukua wanafunzi kwa kuzingatia mahitaji ya hospitali zilizomo vijijini, ili wanafunzi wakimaliza masomo warudi huko pamoja na ugawaji waliohitimu lazima ukubalike na kwamba kufanya kazi ni Unguja na Pemba.
Kwa upande wa wahitimu hao wamesema kuwa licha ya kupewa elimu bora lakini bado chuo hicho kinakabiliwa na upungufu wa walimu hasa kwa kada za maafisa watabibu, maafisa maabara na maafisa wa madawa ukilinganisha na ongezeko kubwa la wanafunzi na ushindani wa vyuo kitaifa na kimataifa.
Wamesema Chuo kinakabiliwa na upatikanaji wa vifaa muhimu ikiwemo vya kujifunzia vya nadharia na vitendo pamoja na vitabu vya kutosha.
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa Chuo hicho, Dk. Hakim Mohammed Bilali amesema wamepania chuo kukifanya cha kisasa licha ya changamoto mbali mbali zinazoikabili chuo hicho na hivi kimeonesha kukua kitaaluma.
Ameiomba wizara kufanya jitihada ya kupatikana kwa mikopo kwa wanafunzi hao kwani asilimia kuwbwa wanaosoma chuoni hapo ni watoto wa kimasikini.

No comments:

Post a Comment