Hatimaye Bunge laondoa mjadala wa katiba
Na Mwandishi Wetu
HATIMAYE Bunge la Jamhuri ya Muungano, limeridhia kuondosha mjadala wa mswada wa rasimu mchakato wa katiba, baada ya wadau kutoka makundi mbali mbali na wanazuoni na wananchi kushauri uondolewe.
Waziri Mkuu wa Mizengo Pinda juzi akijibu suali la papo kwa papo na Mkuu wa kambi ya Upinzani Freeman Mbowe alisema serikali haiwezi kuuondoa hadi hapo kamati ya Bunge ya katiba sheria na Utawala iwasilishe maoni Bungeni.
Spika wa Bunge la Jamhuri, Anne Makinda, alisema Bunge limeamua kuirejesha rasmu hiyo serikalini ili kutoa muda zaidi kwa serikali ili kuyazingatia maoni ya wananchi katika mabadiliko waliyoyapendekeza yafanyike.
Aisema kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala ya Bunge imeomba kupata muda zaidi wa kuweza kuirudisha rasimu hiyo serikalilini ili iweze kuyatafakari maoni ya wananchi na baadae kamati hiyo iweze kuurejesha mswada na yapatikane maoni zaidi.
Spika Makinda alisema anachukua hatua ya kuondosha m mswada huo kutokana na sheria ya Bunge kumpa mamlaka, ambapo ikiwa ataona kuna jambo lina utata katika rasimu na pindipo kamati ya Bunge ikiwa imeomba muda wa ziada jambo ambalo linakubalika.
Spika Makinda alisema jambo la msingi ambalo serikali itapaswa kulizingatia katika mabadiliko yake ni kuona rasimu hiyo inaandaliwa upya kwa lugha ya Kiswahili ili wananchi wengi waweze kufahamu sambamba na kuweza kutoa mawazo yao.
Aidha Spika huyo alisema jambo jengine ambalo serikali itapaswa kulifanya ni kuona mswada huo unachapishwa katika vyombo vya habari hasa magazeti kwa lengo la kuwawezesha wananchi wengi kuwafikia.
Spika alisema chengine kinachohitaji kufanyiwa kazi, Makinda ni la kutambulisha rasimu hiyo kwa wananchi ikiwa na lengo litalowezesha kukusanya maoni mengi kutoka kwa wananchi.
Alisema hatua ya Bunge kutoa muda zaidi imeridhika na hoja za maoni ya wananchi na kuamua kutoa muda zaidi ikiwa ni hatua itayowezesha kupatikana kwa manufaa juu ya suala hilo na kuwataka wananchi kuona wanatumia fursa hiyo.
Alisema kuondolewa kwa mswada huo kunatoa fursa kwa wananchi kushiriki katika ukusanyaji wa maoni mbele ya kamati ya Bunge na kuhakikisha wanadumisha amani kwani rasimu hiyo itahitaji kupata maoni ya wananchi, wasomi, makundi ya kidini, wanasiasa, viongozi wa serikali, asasi zisizo za kiserikali, Walemavu na watu binafsi.
Alisisitiza kuwa kinachohitajika mijadala hiyo iwe zaidi itayochangia mswada huo na sio kushindana kwa vyama katika majukwaa kwani kinachohitajika kupatikana maoni ambayo yataweza kuwa bora kwa rasimu hiyo.
Alisema kazi kubwa ambayo inahitajika kuona inafanyika ni kuipa ushirikiano Tume hiyo kwa kuwaamini zaidi wanasheria wa Tume hiyo kwa kuielekeza wakitakacho kwani rasimu hiyo sio mali ya chama chochote cha siasa na busara ndizo zinazotakiwa kutumika.
“Tunawaomba wananchi waepuke kutoa maneno ya jazba, Watanzania wote wadumishe amani watoe mapendekezo katika Ofisi yetu”, alisema Makinda.
Alisema Mkutano ujao wa Bunge, itatarajia rasimu hiyo ipelekwe kwa mjadala na kusisitiza kuwa shughuli ya ukusanyaji wa maoni bado itatawaliwa na Bunge na mswada huo kwani haupo serikalini.
Hapa Zanzibar jana Jumuiya ya Uamsho ilitarajiwa kufanya maandamano ambapo tayari Jeshi la Polisi liliyazuia kupinga rasimu hiyo.
Saturday, 16 April 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment