Tuesday, 12 April 2011

MMOJA AFARIKI KWA GARI KASKAZINI.

Mmoja afariki kwa gari Kaskazini


Na Khamis Juma

MTU mmoja amefariki dunia papo hapo na mwengine kulazwa hospitali ya Mnazimmoja baada ya gari kuacha njia na kupinduka huko Kibwengo wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mselem Masoud Mtulia alimtaja mtu aliyefariki kuwa Ahmada Issa Mohammed (31), mkazi wa Vuga mjini Unguja.

Alisema Ahmada ambaye alikuwa dereva wa gari hiyo alifariki papo hapo baada ya gari aliyokuwa akiendesha Mark II, yenye namba za usajili Z.936 AL kuacha njia na kujigonga na kiguzo.

Kamanda huyo alimtaja aliyejeruhiwa katika ajali hiyo na kulazwa hospitali ya Mnazimmoja ni Fatma Mohammed Said (30).

Alisema Ahmada alifika na mauti na Fatma kujeruhiwa katika ajali hiyo ambayo ilitokea majira ya saa 7 usiku wa kuamkia jana.

Mwili wa marehemu huyo alifanyiwa uchunguzi katika hospitali ya Kivunge kabla ya kukabidhiwa kwa jamaa zake kumfanyia taratibu za mazishi.

No comments:

Post a Comment