Ukuaji uchumi kuwiana na kuimarisha maisha
Na Ali Mohamed, Maelezo
WAZIRI wa Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika, Haroun Ali Suleiman amesema serikali ya awamu ya saba inakusudia kuweka uwiano kati ya kukua kwa uchumi na pato la taifa na sambamba na kuimarisha maisha ya wananchi wa kawaida.
Akizindua ushirika wa kilimo cha umwagiliaji Mtwango alisema serikali itawawezesha wananchi kupitia vyama vya ushirika kwa fedha na zana za uzalishaji ikiwemo kilimo ili wananchi hao waweze kuzalisha kutokana na rasilimali zilizopo.
“Uchumi hauwezi kukua kama wananchi wa kawaida masikini, tutahakikisha kukua kwa uchumi na kuongezeka kwa pato la taifa kunakwenda sambamba na kuimarika kwa maisha ya wananchi wa kawaida”, Waziri Haroun alifahamisha.
Alisema serikali inaamini kuwa wananchi wakiwezeshwa wanaweza kushirikiana katika masuala ya maendeleo na uzalishaji hivyo itawapitia nyezo muhimu za uzalishaji kwa lengo na kuondosha umasikini kwa wananchi wa kawaida.
Alisema kama ilivyo kawaida ya viongozi kuwatumikia wananchi, hivyo akiwa Waziri mwenye dhamana ya uwezeshaji wananchi kiuchumi atafanya kila liwezekanalo kuhakisha wananchi wanawezeshwa kiuchumi na wanaondokana na umasikini.
Alisema umasikini utaondoka kwa viongozi na wananchi kushirikina kufanya kazi kwa juhudi na maarifa na kila mtu ahisi kuwa umasikini ni tatizo, mzingo kwa taifa na unatakiwa kuondoshwa.
Akizungumzia maendeleo ya ushirika huo wa kilimo cha umwagiliaji Mtwango, Waziri Haroun alisema sekta ya kilimo ni miongoni mwa maeneo muhimu yanaohitaji kupewa msukumo wa hali ya juu katika kuwawezesha wananchi.
Katika hafla hiyo ya uzinduzi Waziri Haroun aliwakabidhi kadi za uanachama wanachama wapya, kukabidhi mikopo kwa wanachama watatu katika ushirika huo na alitoa ahadi ya kuusaidia shilingi milioni moja.
Nae Mkurugenzi wa Ushirika Khamis Simba, alisema vyama vya ushirika vya uzalishaji na fedha ndivyo vinavyopewa kipao mbele kuwezeshwa kwa mikopo na mafunzo ili viweze kutoa ajira kwa wananchi wengi na kuzalisha kutokana na rasilimali zilizopo.
Katika sisala yao wanaushirika huo wa kilimo cha umwagiliaji walisema pamoja na mafanikio wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa maji tatizo ambalo limechangiwa na ujenzi wa barabara ya Mwera.
Walisema kutokana na ujenzi huo mto wa Mwera ambao ulikuwa unategemewa kupeleka maji katika mashamba ya Mtwango umeharibiwa na maji yamekuwa hayaendi kikawaida.
Hata hivyo wanaushirika hao wameanzisha mdadi wa kuchimbi visima kwa ajili ya umwagiliaji ingawa havitishi kutokana na mahitaji ya maji kuwa makubwa hivyo waiomba serikali kuwasadia.
Pamoja na tatizo la uhaba wa maji wanaushrika hao wanakabiliwa na tatizo la uhaba wa mbolea, matrekta na fedha za kuwakopesha wakulima kuendeleza kilimo.
Thursday, 14 April 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment